BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

KAMPUNI YA MADINI YA BARRICK YAIPA NGUVU SERIKALI YA RAIS MAGUFULI BAADA YA KUKUBALI SHERIA MPYA YA MADINI


Rais John Magufuli akishuhudia Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton akiwa na Afisa Uendeshaji wa Barrick Gold, Richard William huku Waziri wa Sheria na Katiba, Profesa Palamagamba Kabudi na Florens Luoga nao pia wakiweka saini ripoti ya makubaliano baina ya Kamati ya Serikali na timu ya wataalamu wa Barrick Gold kuhusu biashara ya madini, Ikulu jijini Dar es Salaam jana.

TANZANIA sasa itaanza kunufaika na rasilimali zake za madini kupitia Sheria yake mpya ya Madini kuungwa mkono na Kampuni ya Barrick Gold Corporation, iliyoshiriki kwenye mazungumzo ya kamati ya maridhiano baina ya serikali na kampuni hiyo.

Hatua hiyo sasa imeipa nguvu Tanzania kunufaika na asilimia 50 ya faida ya biashara ya madini itakayofanywa na kampuni hiyo nchini, sambamba na serikali kumiliki hisa kwa asilimia 16.


Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa makubaliano kati ya pande hizo mbili mbele ya Rais John Magufuli jana Ikulu, Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi aliyeiongoza timu ya Tanzania, alisema wamefikia hatua nzuri ambayo nchi itaanza kunufaika na dhahabu.

“Hatua tuliyofikia ni nzuri na sasa nchi itaanza kunufaika na madini, ingawa haikuwa kazi rahisi tulichukua takribani miezi mitatu kufikia makubaliano haya, ambayo nchi sasa inakuwa mfano wa kuigwa duniani kwa kusimamia rasilimali zake,” alisema Profesa Kabudi. 


Alisema kwa kuanzia, kampuni hiyo imekubali kulipa dola za Marekani milioni 300 (sawa na Sh bilioni 700) kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo,

TANZANIA sasa itaanza kunufaika na rasilimali zake za madini kupitia Sheria yake mpya ya Madini kuungwa mkono na Kampuni ya Barrick Gold Corporation, iliyoshiriki kwenye mazungumzo ya kamati ya maridhiano baina ya serikali na kampuni hiyo.

Hatua hiyo sasa imeipa nguvu Tanzania kunufaika na asilimia 50 ya faida ya biashara ya madini itakayofanywa na kampuni hiyo nchini, sambamba na serikali kumiliki hisa kwa asilimia 16.

Akizungumza wakati wa kusainiwa kwa makubaliano kati ya pande hizo mbili mbele ya Rais John Magufuli jana Ikulu, Dar es Salaam, Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi aliyeiongoza timu ya Tanzania, alisema wamefikia hatua nzuri ambayo nchi itaanza kunufaika na dhahabu.

“Hatua tuliyofikia ni nzuri na sasa nchi itaanza kunufaika na madini, ingawa haikuwa kazi rahisi tulichukua takribani miezi mitatu kufikia makubaliano haya, ambayo nchi sasa inakuwa mfano wa kuigwa duniani kwa kusimamia rasilimali zake,” alisema Profesa Kabudi.

Alisema kwa kuanzia, kampuni hiyo imekubali kulipa dola za Marekani milioni 300 (sawa na Sh bilioni 700) kama malipo ya kuonesha nia njema ya kufidia fedha zilizotokana na upotevu wa mapato kupitia biashara ya kampuni hiyo, Rais Magufuli alisema huo ni mwanzo mzuri.

Pia alisema wamekubaliana kuunda kamati ndogo itakayoshughulikia masuala magumu, ambayo hayakufikiwa kwa kupitia nyaraka za malipo ili kuona jinsi ya kufikia suluhu.

Malengo ya serikali Akizungumzia malengo matano ya serikali katika majadiliano hayo yaliyozaa matunda, Profesa Kabudi alisema walijipanga kabla ya mazungumzo na kwamba malengo hayo matano yamesaidia nchi kuibuka kidedea.

Aliyataja malengo hayo kuwa ni kuainisha fidia na makosa mbalimbali yaliyofanywa na kampuni tanzu ya Barrick nchini. Pili, kujadili na kuweka mfumo mpya wa uendeshaji wa shughuli za uchimbaji na biashara ya madini ili kuweka mgawanyo sawa wa mapato kati ya serikali na kampuni hiyo.

Tatu, kujadili na kukubaliana muundo na mfumo wa uendeshaji utakaowezesha Tanzania kupata manufaa zaidi kutokana na uwekezaji migodini.

Nne, ni kubadilisha mikataba ya migodi ili iendane na Sheria mpya ya Madini; na tano, ni kuhakikisha wananchi na jamii inayozunguka migodi ya madini inapata manufaa zaidi kutokana na uwepo wake kwenye maeneo yao. Makubaliano na mwelekeo.

Akizungumzia mafanikio na mwelekeo wa ushirikiano baina ya serikali na kampuni hiyo, Profesa Kabudi alisema kampuni hiyo imekubali masharti yote yaliyomo kwenye Sheria mpya ya Madini na wameyaingiza kwenye mfumo wa fedha waliokubaliana.

Katika mfumo wa fedha waliokubaliana, Profesa Kabudi alisema serikali itakuwa inamiliki hisa kwa asilimia 16 kama ambavyo Sheria ya Madini inatamka na ugawaji wa faida ya biashara ya madini utakuwa ni nusu kwa nusu, yaani Tanzania itakuwa inapata asilimia 50 ya faida yote. Kadhalika, makubaliano mengine ni kuwa kuanzia sasa fedha zote za biashara ya madini ya kampuni hiyo zinazofanywa Tanzania, zitakuwa zinawekwa akaunti za benki za nchini.

Pia wamekubaliana kuwa ofisi zao za uhasibu na fedha zilizopo London, Uingereza na Johannesburg, Afrika Kusini zihamishiwe nchini na makao makuu yawe Mwanza, eneo ambalo shughuli za uchimbaji zinafanywa.

Lakini, pia katika mwelekeo mpya wamekubaliana kuanzisha kampuni mpya ya kusimamia na kuendesha migodi itakayoongozwa na Mtanzania na pia kutakuwa na wawakilishi wa Kitanzania kwenye Bodi ya wakurugenzi za kampuni hiyo. 


Aidha, wamekubaliana kuwa kazi za migodi zifanywe na kampuni za kitanzania na watanzania wapate nafasi na kuwa ajira hizo zisiwe na mikataba, bali ziwe ajira za uhakika.

“Katika hili tumekubaliana kuwa wafanyakazi wa migodini wasiishi kwenye kambi za mgodi, bali waishi kwenye makazi yao wawe wanakwenda kazini na kurudi nyumbani jioni, siyo tena kulala kambini,” alisema Profesa Kabudi.

Kutokana na maafikiano hayo, Profesa Kabudi alisema kampuni hiyo sasa inaangalia jinsi ya kujenga barabara ya kwenda mgodini ili kurahisisha usafiri wa wafanyakazi na pia wamekubaliana kutenga bajeti ya kujenga maabara ya kupima makinikia nchini.

Mbali na maafikiano hayo, wamekubaliana kuwa serikali itakuwa na umiliki wa madini mengine yote yatakayopatikana kwenye makinikia ya dhahabu. 


Aidha, Profesa alisema kuanzia sasa kesi zote na mashauri kuhusu kampuni hiyo na serikali zitakuwa zinafanyikia hapa nchini badala ya sasa ambapo kesi hufanywa nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Barrick Gold Corporation, Profesa John Thornton alisema wanamshukuru Rais Magufuli kwa kuhakikisha anasimamia jambo hilo kwa umakini na amefungua ukurasa mpya wa ushirikiano baina yao.

Alisema msimamo wa Rais Magufuli unajenga misingi ya biashara ya kuaminiana na uwazi, ambayo ni muhimu na ya namna yake kwa biashara katika karne hii ya 21.

Alisema Barrick Gold Corporation watazingatia makubaliano haya na wanaamini kuwa yamefungua ukurasa muhimu utakaowezesha kufanya biashara kisasa.

“Tunamshukuru Rais Magufuli, hatua ya majadiliano ni nzuri na umeonesha utetezi wako kwa nchi na rasilimali zake, dunia itatambua juhudi na msimamo wako, na kuanzia sasa uhusiano wetu utakuwa wa uwazi,” alisema Profesa Thornton.

Kamati zilizoundwa Awali, Machi mwaka huu, Rais Magufuli aliteua kamati ya wataalamu wanane watakaofanya uchunguzi kwa lengo la kubaini kiwango cha madini kilichomo katika makontena yenye mchanga wa madini yanayoshikiliwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Hatua hiyo ilikuja baada ya Rais kutembelea bandari na kukuta kontena 20 za mchanga huo zikitaka kusafirishwa nje huku awali ikibainika kontena nyingine 260.

Baada ya kushuhudia kontena hizo, Rais alipiga marufuku usafirishwaji wake Machi 2, mwaka huu na kuunda timu hiyo iliyoongozwa na Profesa Abdulkarim Mruma, Profesa Justinian Ikingula, Profesa Joseph Bushweshaiga, Dk Yusuf Ngenya, Dk Joseph Philip, Dk Ambrose Itika, Mohamed Makongoro na Hery Gombela.

Aidha, baada ya kamati hiyo kutoa ripoti yake iliyoonesha udanganyifu wa kiasi kinachosafirishwa, kamati ya pili iliundwa na Rais kuchunguza masuala ya kisheria na kiuchumi kuhusu mchanga wa madini unaosafirishwa nje ya nchi.

Kamati hiyo iliongozwa na Profesa Nehemiah Osoro, Profesa Longinus Rutasitara, Dk Oswald Mashindano, Gabriel Malata, Casmir Kyuki, Butamo Philip, Usaje Asubisye na Andrew Massawe.

Matokeo ya kamati hizo mbili ndio yaliyozaa kamati ya mazungumzo hayo ambayo imekamilisha kazi jana, ikionesha mwelekeo nzuri kwa Tanzania kuibuka kidedea.
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment