BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DK WILBORD SLAA ATEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA BALOZI, KUAPISHWA IKULU


Aliyekuwa Katibu mkuu wa chama cha upinzani CHADEMA ameteuliwa kuwa balozi na Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Katika taarifa ilitolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu ,Gerson Msigwa, haijataja kituo chake cha kazi. Ila imeeleza "ataapishwa baada ya taratibu kukamilika"

Dokta Wilbord Slaa alikuwa kiongozi muandamizi wa upinzani nchini Tanzania.

Alijiuzulu nafasi ya ukatibu mkuu na uanachama wa Chadema mwaka 2015 baada ya ujio wa waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa ambaye alipewa nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya chama hicho mwaka huo.

Slaa amekuwa katika siasa kwa zaidi ya miongo miwili na kabla ya hapo alikuwa padri wa kanisa katoliki.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: