BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

JENGO LA TANESCO KUBOMOLEWA KWA KUKATA NA KISU KIKUBWA DAR ES SALAAM


WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA), umesema kuna njia tatu za kubomoa majengo marefu lakini iliyo nzuri na inayoweza kutumika kubomoa ghorofa la Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ni kukata jengo hilo kwa visu vikubwa ili kutoa vipande vipande.

TBA imesema njia hiyo ni salama zaidi kwa wakazi wanaolizunguka jengo hilo, kulinganisha na njia za upigaji wa baruti au mabomu.

Mtendaji Mkuu wa TBA, Elius Mwakalinga aliyasema hayo jana wakati akizungumza na Nipashe lililotaka kufahamu ni njia gani bora ya kutumika kubomoa jengo la ghorofa tisa la Tanesco baada ya agizo la Rais John Magufuli wiki iliyopita kuwa libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara za juu za Ubungo.

Rais Magufuli alitoa agizo la ubomoaji wa jengo hilo wiki ilyiyopita alipowasili jijini Dar es Salaam akitokea mapumzikoni Chato, mkoani Geita.

Rais Magufuli alimwagiza Meneja wa Wakala wa Barabara (Tanroads) Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Ndyamukama Julius kuvunja sehemu ya jengo la Tanesco na jengo la Wizara ya Maji ili kupisha ujenzi wa barabara za juu.

Rais Magufuli alisema Sheria ya Hifadhi ya Barabara katika eneo la Ubungo ni mita 90 kila upande kutoka katikati ya barabara, hivyo ni lazima sheria hiyo iheshimiwe ili kuharakisha ujenzi wa daraja la ghorofa tatu bila kikwazo, na kwamba sheria ni msumeno.

"TBA bado hatujapata taarifa za kuhusika kubomoa jengo hilo, lakini kuna njia tatu za kubomoa jengo refu," alisema Mwakalinga.

"Ya kwanza ni mlipuko au mabomu kutumika, ya pili ni kukata kwa kutumia visu vikubwa na 'crane' ukitoa mapande."

"Njia ya tatu ni ya kienyeji ambapo tunatumia tindo, ila njia hii siyo nzuri sana kwa majengo makubwa."

Mwakalinga alisema kwa jengo la Tanesco, njia ya kukata kwa kutumia visu vikali na vikubwa ni rafiki hata kwa majengo yanayolizunguka, pia haina madhara.

Alisema njia ya mlipuko ina gharama kwa sababu itahitajika kuwahamisha majirani na wakati mwinginge kusababisha majengo ya jirani kupasuka au kupata nyufa.

"Wagonjwa wa moyo hawawezi kuathirika ukitumia njia ya kukata kwa visu vikubwa, tofauti na njia ya kulipua," alisema zaidi Mwakalinga.

Naye Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi (AQRB), Mhandisi Albert Munuo alisema Tanesco wanapaswa kuwashirikisha wataalam katika kubomoa jengo hilo ili kusitokee madhara.

"Huwezi kubomoa kienyeji kwa sababu utaleta madhara kwa majirani na wapita njia, ukibomoa kienyeji mali zinaweza kuharibika," alisema Mhandidi Munuo. 


Alipoulizwa ni njia gani ambayo ni salama zaidi, Mhandisi Munuo alisema wataalam watakaoteuliwa kufanya kazi hiyo ndiyo watakaoshauri njia bora ya ubomoaji.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: