BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MABINGWA WA SOKO MKOA WA MOROGORO SHUPAVU FC WATUPWA FAINALI ZA RWAKATARE CUP 2017

Mbunge wa kuteule mkoa wa Morogoro, Mchungaji Getruda Rwakatare akipiga mpira na kufunga bao kwa njia ya mkwaju wa penalti kama ishara ya ufunguzi mashindano ya Rwakatare Cup 2017 yaliyoshirikisha jumla ya timu za soka 80 kijiji cha Mng'eta uwanja wa Lukolonga wilayani Kilombero mkoa hapa, wa pili mwenye kofia nyekundu ni Mkuuu wa wilaya ya Kilombero, James Ihunyo. 

Juma Mtanda, Morogoro.
Mabingwa wa soka mkoa wa Morogoro msimu wa 2017/2018, timu ya Shupavu FC imeshindwa kutinga nusu fainali ya Rwakatare Cup 2017 baada ya kukumbana na kipigo cha bao 5-3 mbele ya vijana machachari wa Idete FC.

Shupavu FC ilikumbana na kipigo hicho wakati wa mchezo mkali wa robo fainali uliopigwa jana kwenye dimba la shule ya msingi Lukolongo kijiji cha Mngeta wilaya ya Kilombero mkoani hapa.

Ndoto za mabingwa hao kuwa mabingwa wa Rwakatare Cup 2017 zilishindwa kutimia baada ya kujikuta wakienda sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 kabla ya kuondoshwa kwa kutandikwa bao 5-3 kwa njia ya penati huku kipa wa Idete FC, Mohamed Ngozi akiwa kikwazo kwa Shupavu FC kutinga nusu fainali hizo kufuatia kudaka penalti mbili.

Akizungumza na gazeti hili mkoani hapa, Msimamizi mkuu wa Rwakatare Cup 2017, Supertus Duma alisema kuwa Idete FC imefuzu na kutinga nusu fainali baada ya kuwatandika mabingwa wa soka wa mkoa wa Morogoro Shupavu FC kwa penati 5-3 baada ya kumalizika kwa dakika 90 bila kufungana wakati wa mchezo wa mwisho wa robo fainali.

Duma alitaja timu nyingine zilizofuzu kuingia nusu fainali kuwa ni JKT Chita FC iliyopata ushindi wa bao 1-0 mbele ya Mngeta Rangers FC wakati Melela Express FC imesonga mbele kwa kuilaza City Boys FC 2-1 na Super Mahakama FC ilitinga nusu fainali bila jasho baada ya timu ya Teachers FC ya Mlimba kushindwa kutokea kwenye mchezo wao war obo fainali.

“Nusu fainali ya kwanza Rwakatare Cup 2017 itawakutanisha timu ya Super Mahakama FC dhidi ya JKT Chita FC leo (jana) na nusu fainali ya pili itakuwa kati ya timu ya Melela Express FC na Idete FC (leo jumatano).alisema Duma.

Duma alisema kuwa fainali za mashindano hayo yatapigwa Novemba 24 mwaka huu na bingwa wa kihistoria atakabidhiwa zawadi ya fedha taslimu sh2 milioni wakati mshindi wa pili atapata zawadi ya fedha ya sh1milioni.

Mashindano hayo yalianza kutimua vumbi julai 21 mwaka huu ikishirikisha jumla ya timu 80 ambazo ziligawanywa kwenye vituo saba vya Chita, Mngeta, Mlimba, Mkamba, Namawala, Ifakara na Mang’ula na kupata timu mbili zilizoingia kwenye hatua ya 16 bora.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: