BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MBUNGE WA SONGEA MJINI , LEONIDAS GAMA KUZIKWA JUMATATU MAKABURI YA FAMILIA


Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini, Leonidas Gama akipimwa afya na Muuguzi Asha Shao bungeni Dodoma. picha maktaba.

SONGEA.Mbunge wa Songea Mjini kupitia CCM, Leonidas Gama amefariki dunia katika hospitali ya Peramiho mkoani Ruvuma akipatiwa matibabu na kutarajiwa kuzikwa Jumatatu katika makaburi ya familia yaliyopo Kijiji cha Likuyufusi mkoani Ruvuma.

Taaifa za kifo cha Mbunge huyo zimethibitishwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Oddo Mwisho, na kueleza marehemu amefariki dunia usiku wa saa 6 kuamkia leo Novemba 24,2017.

Mwisho amesema kwa kusema kwamba alipata taarifa kwamba Leonidas Gama alianguka ghafla usiku wa jana kutokana na tatizo la presha na kukimbizwa hospitali ya Peramiho, mpaka pale umauti ulipomkuta.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: