BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS ROBERT MUGABE AJIUZULU KWA SHINGO UPANDE URAIS WA ZIMBABWE.

 
Katika dakika chache zilizopita , spika wa bunge la Zimbabwe ametangaza kuwa rais Robert Mugabe amejiuzulu .

Spika wa bunge, Jacob Mudenda alisema kuwa hatua hiyo ni ya kujitolea na amefanya hivyo ili kuweza kuwepo kwa mabadiliko mazuri ya mamlaka kulingana na chombo cha habri cha reuters.

Tangazo hilo la ghafla lilizuia harakati za bunge kutaka kumng'oa madarakani ambazo zilikuwa zimeanza dhidi yake.

Kwa mujibu wa chombo cha habari cha Reuters, Spika wa bunge amesema kuwa kiongozi mpya atawekwa madarakani siku ya kesho Jumatano.

Wabunge walifurahia kufuatia hatua hiyo na raia wameanza kusherehekea barabarani.

Awali Robert Mugabe alikuwa amekataa kujiuzulu licha ya jeshi kuchukua mamlaka huku hatua hiyo ikifuatiwa na maadamano ya raia waliotaka kiongozi huyo kung'atuka mamlakani wiki hii.BBC
Share on Google Plus

About Juma Mtanda

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
Post a Comment