BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MWANAMUZIKI WA KIKE AFUNGWA MIAKA MIWILI JELA KWA KULA NDIZI BAADA YA KUONEKANA KATIKA VIDEO

Shyma appears in the video for I Have IssuesMahakama nchini Misri inaripotiwa kumfunga mwimbaji mmoja miaka miwili jela baada ya kuonekana kwenye video moja ya mziki akiwa na vazi la ndani huku akila ndizi.

Shaimaa Ahmed, 25, ambaye kimuziki anafahamika kama Shyma, alikamatwa mwezi uliopita baada ya video hiyo kuzua ghadhabu kwenye taifa hilo.

Siku ya Jumanne alipatikana na hatia ya kuunga mkono mapenzi na kwa kuchapisha video inayokiuka maadili.

Mwelekezi wa video pia naye alihukumiwa kifunga cha miaka miwili licha ya yeye kutowepo mahakamani.

Shyma alikuwa ameomba msamaha kabla ya kukamatwa kwake.
"Sikufikiria haya yote yatafanyika na kwamba ningeshambuliwa kwa njia hii kali kutoka kwa kila mtu."

Mwaka uliopita mahakama nchini Misri ilawahukumu wacheza dansi watatu wanawake miezi sita gerezani baada ya kuwatuhumu kwa kuchochea ngono kwenye video ya muziki.

Mwimbaji mwingine anakabaliwa na kesi kwa kueneza uvumi kuwa maji ya mto Nile yanaweza kumfanya awe mgonjwa.BBC
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: