BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAFURIKO YAWAVURUGA WAATHIRIKA, VIONGOZI WAHAHA KUWANUSURU NA MLIPUKO WA MAGONJWA KILOSA MOROGORO

Mhandisi mkuu wa shirika la reli Tanzania (TRL), Nelsoni Ntego (Mwenye sharti nyeupe) afafanua jambo wakati kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Morogoro ilipotembelea eneo la Mkadage moja ya maeneo miundombinu ya reli imeharibiwa na maji ya mafuriko yaliyopasua kutoka kwenye mto Mkondoa wilaya ya Kilosa.Picha na Juma Mtanda. 

Juma Mtanda, Morogoro.
Mafuriko yaliyoikumba wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro yamendelea kuathiri shughuli mbalimbali za kiuchumi huku halmashauri hiyo ikihaha kwa kuanza kugawa viwanja vya makazi kwa wananchi waliokuwa wanaishi kwenye maeneo hatarishi wilayani humo.

Athari kutokana na mafuriko hayo zimeongezeka ambapo idadi ya kaya zilizopoteza makazi zimeongezeka kutoka 1,831 na kufikia idadi ya kaya 2,701 zenye watu 9,345.

Kufuatia athari hizo Halmashari ya Wilaya ya Kilosa inatarajia kugawa viwanja 2400 kwa wahanga wa mafuriko wilayani humo.

Akizungumza na MTANDA BLOG wilayani hapa, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Kilosa, Kessy Mkambala alisema kuwa mpaka sasa tayari nyumba 377 zimebomoka na nyumba nyingine 2,266 zimezingirwa na maji ya mafuriko.

Kata zilizoathiriwa ni pamoja na Mkwatani, Chanzuri, Berega, Kidete, Magomeni, Masanze, Mbumi, Tindiga, Mbigiri na Mabwerebwere.

Mkambala alisema kuwa kutokana na idadi kubwa ya watu kuathirika, halmashauri mpaka sasa tayari imepokea misaada mbalimbali kwa lengo la kuwagawia waathirika ikiwemo tani 16 za mahindi, sembe 407, mchele kg 20 na sukari kg 20.

Vingine ni fedha sh 5.5milioni, dawa za kutibu maji vidonge 360, sabuni katoni 10 na maji katoni 87 huku halmashauri ikiwa imetenga viwanja 2400 kwa ajili wa watu ambao nyumba zao zimeathirika na mafuriko hayo.alisema Mkambala.

Kwa upande wa mbunge wa jimbo la Mikumi, Joseph Haule (Profesa Jay) alieleza wananchi wa vijiji vya Tindiga na Mabwerebwere kuwa wakubaliane na mpango wa serikali wa kuhama na kwenda kuanza makazi mapya katika maeneo salama.

Haule alisema hayo jana, wakati akiwapa pole wananchi wa vijiji hivyo na kutoa msaada wa chakula tani mbili na nusu za unga sembe.

Haule alisema kuwa hali ni mbaya kwa vijiji vya Tindiga na Mabwerebwere baada ya kutokea kwa athari za mafuriko yaliyoanza Januari 8 hadi 12, mwaka huu hivyo wananchi wote kuna haja wa kukubaliane na mpango wa serikali wa kuhama maeneo ambayo yameonekana si salama kwa maisha yetu.

Aliongeza kwa kusema kuwa kwa shule zilizoathirika na mafuriko wanafunzi wake, wahamishiwe kwenye vijiji vya jirani ili watoto hao wasiendelee kukaa bila kusoma wakati serikali ikijipanga zaidi kutatua changamoto zikiwemo cha wanafunzi.alisema Haule.

Mkazi wa Kilosa, Esther John alisema kuwa mafuriko hayo yameathiri kwa kiasi kikubwa shamba lake la mpunga la heka moja na nusu baada ya maji yenye tope kufunika zao hilo ambalo alitarajia kuvuna mwezi wa nne mwaka huu.

“Sijui nifanye nini ?..kwani mipango yangu yote imekwama na nilitegemea mpunga nianza kuvuna mwezi wa nne lakini maji ya mafuriko yaliyochanganyika na matope imefunika mpunga wote ambao ulikuwa umefikia kwenye magoti onde la Mkadage.”alisema Eshetr.

Mafuriko yanaathiri Kilosa yanatokana na mvua zinazonyesha mikoa ya Dodoma na Manyara na kusababisha maji kujaa Mto Mkondoa kubomoa sehemu za kingo la tuta na kuingia katika makazi ya watu na mashamba katika vijiji hivyo wilayani hapa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: