Wafanyakazi wa mfuko wa mashiriki ya umma kanda ya mashariki na kati (PPF) Paulina Msanga kulia na Jeniffa Honest wakicheza musiki wakati wa hafla ya uanzishwaji wa klabu za michezo ikiwemo soka, netiboli na basketiboli kwa taasisi tatu za benki ya KCB Tanzania Morogoro na mfuko wa taifa wa bima ya afya katika ukumbi wa Madagu Mess mkoani Morogoro.
Meneja wa mfukomashiriki ya umma kanda ya mashariki na kati (PPF), John Mwalisu akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo.
Meneja Mwandamizi wa benki wa KCB tawi la Morogoro Hogla Laiser akieleza jambo katika hafla hiyo.
Meneja wa mfukomashiriki ya umma kanda ya mashariki na kati (PPF), John Mwalisu katikati akimkabidha zawadi ya fulana, Taph Tweve kulia kutoka benko ya KCB Tanzania tawi la Morogoro baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika shindano la unywaji kinywaji kwa mrija na kushoto ni Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya Morogoro, Rose Ongara.
HABARI KAMILI YA HAFLA HIYO ENDELEA KUIPATA
WAFANYAKAZI wa taasisi tatu tofauti katika mkoa wa Morogoro zinatarajia kuunda klabu ya michezo kwa lengo la kuimarisha afya na kuweza kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya mkoa huo.
Hayo yalizungumzwa na viongozi wa taasisi za Benki ya KCB Tanzania tawi la Morogoro, mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) na mfuko wa taifa wa bima ya afya wakati wa hafla ya mpango huo katika ukumbi wa Magadu Mess mjini hapa.
Lengo la kuanzisha kwa michezo hiyo kwa taasisi hizo zitasaidia kufahamiana baina ya wafanyakazi, kubadilishana mawazo na itasaidia kujenga umoja na mshikamano baina ya taasisi hizo.
Afisa Mwendeshaji mfuko wa pensheni kanda ya mashariki na kati (PPF) Astronaut Liganga alisema lengo la kuanzisha michezo baina ya taasisi hizo zitasaidia kujenga umoja, mshikamano na wafanyakazi kuimarisha afya zao kupitia michezo.
Liganga alisema kuwa michezo ambayo itaanzishwa kwa sasa ni pamoja na soka, netiboli na basketiboli na kuwa baada ya kukubaliana na wazo hilo viongozi wakuu watakaa na kuujulisha rasmi uongozi wa juu ili nao waweza kutia baraka zao.
Alisema kuwa hili wazo ni zuri sana hivyo ni namna ya kuanzisha na namna ya kupata fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya michezo hiyo hivyo kwa upande wake atachukua jukumu la kusimamia mchezo wa soka na kudai kuwa Meneja wa mfuko wa bima ya taifa ya afya Morogoro, Rose Ongara ataongoza jahazi la michezo ya netiboli na basketiboli.
“Sisi tutakuwa viongozi wa muda wa michezo hii ukiangalia mama yetu Ongara amewahi kucheza michezo hiyo na mimi nimewahi kucheza soka hivyo mpango uliopo kwa sasa ni kujipanga na kuandaa bonanza ambalo litajumuisha michezo yote na lengo la hili ni kupata vipaji ndani ya taasisi zetu nina imani kuna vipaji vingi vimejificha ndani KCB, PPF na mfuko wa bima ya taifa ya afya tutaviibua” alisema Liganga.
Naye Meneja wa mfuko wa bima ya taifa ya afya Morogoro, Rose Ongara alisema kuwa kwa upande wa mchezo wa netiboli na basketiboli ana imani ya kupata wachezaji wazuri kwani kuna mabinti wenye umbo zuri la kucheza netiboli na baskeboli.
Ongara alisema kuwa mpango huo utakapo kamilika wanatarajia kuibua vipaji kwa michezo yote ya soka, netiboli na basketiboli na litasaidia kuongeza mshimano baina ya wafanyakazi wote wakiwemo na viongozi wa taasisi hizo.
Katika hafla hiyo ambayo ilishirikisha viongozi wakuu wa taasisi hizo wakiwemo mameneja na wasaidizi wao wakiwemo na wafaanyakazi wa kila idara.
0 comments:
Post a Comment