Arusha, Tanzania
WAKATI watanzania wakiendelea kufuatilia tukio la kunyongwa kwa watanzania wawili waliokamatwa na dawa ya kulevya nchini Misri, ndugu wa mmoja wa watuhumiwa katika kesi hiyo ameeleza masikitiko yake juu ya kukamatwa kwa ndugu yake.
Watanzania hao (mmoja pichani) wakazi wa Jiji la Dar es Salaam walikamatwa nchini humo wakiwa na dawa za kulevya na kufikishwa Mahak
amani ambapo ilielezwa kwamba hukumu yao ilitarajiwa kutolewa leo na kupelekwa moja kwa moja kwenye chumba cha kunyongwa.
Akizungumza na Habarimpya.com akiwa jijini Arusha mmoja wa ndugu wa watuhumiwa hao alidai kwamba taarifa za kunyongwa kwa ndugu yao walizipata kupitia vyombo vya habari na kwamba waliweza kuwasilia na Serikali kupitia Ubalozi wa Tanzania nchini humo na kupewa taarifa kamili juu ya tukio hilo.
"Mpaka hivi sasa hatuna uhakika kwamba wameshanyongwa ama bado,ingawa taarifa tuliyokuwa nayo ni kwamba sheria za nchi hiyo zinaruhusu mtuhumiwa yeyote wa dawa za kulevya kuhukumiwa ndani ya wiki moja na adhabu yake ni kunyongwa ambapo inatakiwa itekelezwe ndani ya saa 48 baada ya hukumu kutolewa"alisema mmoja wa ndugu wa watuhumiwa hao.
0 comments:
Post a Comment