BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MGOMBEA URAIS UKAWA APIGWA STOP UZINDUZI JANGWANI



Jiji la Dar es Salaam wamemzuia Mgombea wa UKAWA, Edward Lowassa kuzindua kampeni yake kwenye viwanja vya Jangwani Jumamosi ya 29 Agosti , 2015.


Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA , James Mbatia amesema jiji umewagomea kufanya uzinduzi huo Jangwani kwa madai kuwa tayari kuna mtu mwingine ambaye ameshalipia uwanja huo.


Mbatia anasema pamoja na kufanya juhudi za kuomba kutajiwa aliyelipia uwanja huo ili wazungumze naye , Jiji walikataa.


Mbatia anasema viongozi wengine wa UKAWA wanashughulikia suala hilo ikiwa pamoja na kumtaka Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Damian Lubuva kuingilia kati.


UKAWA umesisitiza kuwa wataendelea na ratiba yao kama ilivyopangwa .

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: