Kufuatia tukio la kighaidi katika jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Abuja, Ijumaa 26 Agosti 2011, Jumamosi mara baada ya kupata taarifa hiyo , Baba Mtakatifu Benedikto xv1, alionyesha masikitiko yake kwa tukio hilo, na kupeleka salam zake za rambirambi kwa watu wenye mapenzi mema wa Nigeria, kupitia kwa Rais wa Goodluck Jonathan wa Nigeria na kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon.
Telegramme hizo zilizotumwa na Katibu wa Nchi ya Vatican , Kardinali Tarcisio Bertone, kwa niaba ya Papa. Kardinali Bertone, ameeleza jinsi Papa alivyoguswa na taarifa hizo mbovu za shambulio la Kighaidi , ambamo maisha ya watu yameangamizwa.
Papa ameonyesha kushikamana na Wanageria wote wenye mapenzi mema, katika kuomboleza vifo vilivyotokea , na kuwataka wale wote wanaochagua njia ya kifo na ghasia , kwa lengo la kufanikisha nia zao binafsi, kusitisha utendaji huo na kuheshimu thamani ya maisha ya binadamu . Amewetaka wafuata njia ya majadiliano iwapo kuna yanayowakera.
Papa anaziombea roho za wote waliokatishwa maisha yao katika tukio hili , pia baraka na faraja za Mwenyezi Mungu, kwa familia zilizopoteza wapendwa wao katika tukio hili na kwa wote waliodhurika au kuteswa kwa amna moja au nyingine na dhuluma hii.
Telegramme kama hiyo pia ilitumwa kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , Bwana Ban ki Moon, akimpa pole na kumfariji, Mtendaji Mkuu wa Shughuli za Umoja wa Mataifa, ambaye ameguswa moja kwa moja, kwa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa kupoteza maisha katika tukio hilo la Kighaidi.
Shambulio hilo lililofanyika siku ya Ijumaa katika jengo la Ofisi za Umoja wa Mataifa mpaka siku ya Jumamosi kulitajwa watu ishirini kupoteza maisha. Na ilikuwa bado kujulikana kama bomu hili lilikuwa ni bomu la kamikaze au kama ni utendaji wa kikundi cha Boko Haram, kinachotafuta kuitawala Nigeria yote wka sharia za Kiislamu.
Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulio hili la bomu lilitengwa kwenye gari, na kulipuka, likiharibu jengo la ofisi za idara na mashirika ya Umoja wa Mataifa, lililoko kwenye mji mkuu Abuja.
Akizungumzia tukio hilo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa kitendo hicho ni dhihaka dhidi ya watu waliojitolea kwa ajili ya kuwasaidia watu wengine. Na kwamba, amemtuma msaidizi wake Asha-Rose Migiro kwenda Nigeria, kutathimini athari zake.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment