CHEKA NA MAUGO.
KAMA VILE CHEKA KUSHOTO AKIMNONG'ONEZA MAUGO KWA KUSEMA HIVI "KUWA NITAKUPIGA KWA POINTI USIHOFU MAUGO NITAKULINDIA HESHIMA YAKO SAWA MAUGO ILA USINIKUMBATIE SANA MASHABIKI WATAJUA TUMEPANGA MATOKEO.
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Francis Cheka (SMG) ameendeleza wimbi lake la ushindi baada ya kumtwanga Mada Maugo kwa pointi 100-98 katika pambano lisilokuwa na ubingwa lililofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro.
Katika pambano hilo lililoshuhudiwa na waandishi wa BLOGU HII katika uwanja huo wa jamhuri ambalo lilihudhuriwa na mashabiki lukuki wa mchezo wa ndondi kutoka mikoa mbalimbali ya jirani na viunga vya Manispaa ya Morogoro lilivuta hisia kutokana na mabondia hao kuwa na kiwango kizuri cha masumbi hapa nchini kwa kujiuza maswali yupi ataweza kuibuka kidedea katika pambano hilo.
Baada ya kuanza kwa pambano hilo lililokuwa likichezeshwa na mwamuzi Nemes Kavishe lilianza kwa Cheka kusukuma konde kwa mpinzani katika mzunguko wa kwanza na wa pili kabla ya Maugo kujibu mashambulizi katika mzunguko wa tatu na nne katika mpambano uliokuwa na mizunguko 10.
Maugo alionyesha upinzani mkali katika mzunguko wa tatu na nne kwa kurusha makonde mazito yaliyomfanya Cheka kujihami kwa kumkumbatia katika ajabadilisha hali ya mchezo katika mchunguko wa tano, sita, saba katika mzunguko huyo aliweza kumtandika Maugo na katika mzunguko wa tano alidondoka chini baada ya kutwanga ngumi nzito na mpinzani wake.
Cheka kabla ya kuanza kwa mzunguko wa sita alinyanyua mikono juu kuonyesha ishara ya mashabiki kushangilia huku wakiimba Cheka, Cheka, Cheka hali hiyo iliwachanganya mashabiki wachache wa Maga Maugo kushindwa kumshangilia bondia wao ambapo hali hiyo ilimpa morali Cheka kuendelea kuonyesha umahili wake mzunguko wa sita, saba na nane huku mpinzani wake kushindwa kuonyesha upinzani.
Maugo ambaye muda mwingi alikuwa akijihami kwa kumkumbatia Cheka aliendeleza unyonge katika mzunguko wa tisa kwa kuruhusu makonde ya Cheka kutua katika uso wake ambapo katika mzunguko wa 10 alionyesha katika dakika ya kwanza aliweza kumtwanga ngumi mfulululizo mpinzania kwabla ya dakika zilizosalia kudhibitiwa tena na Cheka hadi kengele ya kumaliza mpambano huo.
Majaji watatu wa mpambano huo walimpa Francis Cheka pointi 99-98, 100-98 na 99-99 na katika michezo ya utangulizi Juma Kihiyo Morogoro aliweza kumtwanga Joseph Sinkara Dar es Salaam kwa KO katika mzunguko wa pili wa mizunguko sita, Deo Njiko aliweza kumtwanga mpinzani wake mkuu Maliki Kinyogoli kwa pointi baada ya kupata 79-77, 50-78 na 79-78.
Bondia Obote Ameme Dar es Salaam alishindwa kutokea ulingoni dhidi ya Seba Temba Morogoro na Sadiki Abdalah na Fadhil Magia wote kutoka jijini Dar es Salaam walishindwa kutambiana baada ya kumaliza mchezo wao wa mizungo sita kwa kuvungana poniti baada ya majaji kutoa 59-58,59-59 na 57-58.
Katika mpambano huo ulimbwa na kikundi cha TMK chini ya kiongozi msanii Juma Kassim Nature.
0 comments:
Post a Comment