BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKUU WA WILAYA MOROGORO KUMGHARAMIKIA ALIYEVUNJWA MKONO NA WAFUGAJI KIJIJI CHA KONGWA.


Seleman Malo (33) mkazi wa kijiji cha Kongwa tarafa ya Mvuha akionyesha mkono wake wa kulia uliovunjwa na wafugaji jamii ya kisukuma.


MKUU wa wilaya ya Morogoro Saidi Mwambungu amejitolea kugharamia matibabu ya mwananchi wa kijiji cha Kongwa tarafa ya Mvuha kilichopo wilayani humo anayedaiwa kuvunjwa mkono na wafugaji wa kabila la kisukumu katika mapigano na wakulima yaliotokea kijijini hapo hivi karibuni mkoani hapa.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa kijiji cha Kongwa septemba 3 mwaka huu Mwambungu alisema amejitolea kumgharamia ghalama za matibu za mwananchi Selemani Kibwana Malo (33) baada ya kuona mkono wake wa kulia kuvunjwa na wafugaji wa jamii ya wasukuma ambapo majeruhi mwananchi huyu alishindwa kumudu ghalama za matibu hospitalini na kukaa bila matatibabu kwa zaidi ya miezi nane tangu kuvunjwa mkono huo.

Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya ya kujitolea matibabu ilitokana na malalamiko yaliyotolewa kwake na wananchi mbalimbali waliojeruhiwa katika mkutano wa hadhala na wakulima wa kuwataka kuacha vurugu za kutaka kulipiza kisasi dhidi ya wafugaji kuwa walipata mateso kutoka kwa wafugaji hao kutokana na kupigwa na kujeruhiwa kwa nyakati tofauti wakati wa wafugaji wakilisha mifugo katika mashamba ya wakulima hao.

Mwambungu aliwaeleza wananchi hao kuwa kipindi hiki serikali imejipanga kuondoa kabila kero hiyo na kuwataka kutulia kwani ipo katika mchakato wa kuhahakiki upya idadi ya wafugaji wa kigeni walioingia kijijini hapo kihalali na wataobainika kuingia kinyume na taratibu za kijiji wataondolewa na kurudi walikotoka.

Naye kijana Selema Kibwana Malo alimweleza mkuu huyo kuwa alivunjwa mkono Februari 10 mwaka 2010 majira ya mchana wakati wachungaji wa jamii ya wasukuma kuingiza mifugo katika shamba lake la mahindi na kunde ambapo aliwataka vijana hao kuwaondoa mifugo yao shambani lakini walikaidi amri hiyo.

Aliendelea kumueleza kuwa katika mabishano hayo mwananchi huyo alichukua maamuzi ya kuwaondoa mifugo hiyo shambani ili wasiendeleaa kuharibu mazao yake lakini alikabiliana na upinzani mkali kutoka kwa vijana hao na kuanza kumshambulia kwa kumchapa na fimbo na hatimaye kufanikiwa kumvunja mkono wake wa kulia katika mapigono hayo yaliyodumu kwa zaidi ya dakika 10 ambapo baada ya kipigo hicho mkulima huyo alipoteza fahamu kabla ya wanancni kujitokeza kutoa msaada huku vijana wa kifugaji wakiwa wametokomea eneo jingine.

“mkuu wa wilaya huu mkono nimevunja na vijana wa jamii ya wafugaji tangu Februari 10 mwaka 2010 lakini mpaka leo hii nimeshindwa kumudu matibabu kutokana na familia yangu kushindwa kumudu ghalama za matibabu hivyo naomba unisaidi ili nipate matibabu ya mkono wangu huu uliovunjika”. Alisema Malo.

Wakati huo huo Afisa Mtendaji wa kijiji cha Kongwa Tarafa ya Mvuha wilaya ya Morogoro Vijijini Rajabu Mkumba aliliambia gazeti hili kijijini hapo hivi karibuni kuwa jumla ya wakulima 15 wa kabila la wakutu walijeruhiwa vibaya na wafugaji wa jamii ya kisukuma kutokana na tabia za wafugaji hao kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima na pindi wakulima wanapojitokeza kukamata au kuwaondoa mifugo hiyo sambani wamekuwa wakikabiliana na upinzani mkali ikiwemo kupigwa na wafugaji hao.

Alisema tangu ameingia madarakani mei mwaka huu ofisi yake ilipokea mashkata matano ya wakulima dhidi ya wafugaji wa jamii ya kisukuma wakilalamikia vitendo vya wafugaji hao kuwapiga wakulima na kuwajeruhi wakati wakijaribu kuondoa mifugo shambani au kuwakamata kwa lengo la kutaka kulipwa fidia ya kuharibiwa mazao yao.

Afisa huyu mtendaji wa kijiji cha Kongwa aliendeleza kulieza gazeti hili kuwa zaidi ya wakulima 10 walijeruhiwa na wafugaji kabla ya kuingia katika madaraka hayo kwa kuona wananchi hao wakiwa wamejeruhiwa na wafugaji hao.

Afisa Mtendaji huyo alisema kuwa mgogoro uliopo kati ya wafugaji na wakulima umechangiwa na viongozi wa serikali ngazi ya kijiji cha Kongwa, kata ya Mvuha na tarafa ya Mvuha wilaya Morogoro Vijijini kutokana na kushindwa kusuluhisha kikamilifu malalamiko ya wakulima dhidi ya wafugaji kwa madai ya wafugaji wengi wameingia kijijini hapo kinyume na taratibu za kijiji ikiwemo mkutano mkuu ambao ndiyo una mamlaka ya kupokea wageni na kukataa.

Viongozi wanadaiwa kuegemea upande wa wafugaji kutokana na madai ya kupokea zawadi mbalimbali za wafugaji wa jamii ya wafugaji ambapo kitendo hicho kimechangia wakulima kuhisi kushindwa kutatua kero zinazowafikia ofisini kwao kutokana na zawadi hiyo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: