BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

Walimu wa shule za umaa wanaza mgomo Kenya.


Wanafunzi wa Kenya wamekusanyika katika shule ya msingi ya Kongoni mjini Nairobi, Kenya, baada ya shule kufunguliwa kote nchini, Jan. 14, 2008.

Walimu wa shule za msingi na upili wamenaza mgomo wa kitaifa kudai kuajiriwa kwa walimu zaidi kukabiliana na muongezeko mkubwa wa wanafunzi.

Wajumbe wa serikali na viongozi wa chama cha walimu wameshindwa kukubaliana juu ya madai ya kuajiri walimu zaidi kukidhi mahitaji ya masomo nchini Kenya.

Waziri mkuu Raila Odinga alikutana Jumatatu na viongozi wa chama cha waalumu katika juhudi za mwisho kujaribu kuzuia mgomo huo kuendelea, lakini walimu wanashikilia kwamba serikali inabidi kuajiri takriban walimu elfu 19.

Mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Nairobi Mwai Gikonyo anaripoti kwamba tatizo kubwa ni kwamba fedha zilizotengwa kuwalipa walimu wepya zimetumiwa kulipa madeni ya wabunge.

Kwa upande mwengine vyanzo vya habari vinaeleza kwamba fedha hizo za waalimu zimetumiewa pia kulipa nyongeza ya mishahara ya wanajeshi.

Akizungumza na sauti ya amerika mwalimu washule ya msingi ya Nivasha Esther Njuguna anasema tatizo kubwa ni kwamba hawana walimu wa kutosha kukabiliana na idadi kubwa ya wanafunzi. Anasema kwa wastani darasa moja inakaribu wanafunzi mia moja kwa mwalimu mmoja.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: