BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

BARAZA LA MAASKOFU KIPENTEKOSTE TANZANIA LAUNGA MKONO SERIKALI KUPINGA VITENDO VYA USHOGA NA NDOA ZA JINSIA MOJA.


Mwenyekiti wa baraza la maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT) Askofu David Batenzi kushoto akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati barabza hilo likitoa tamko juu ya kuungana na serikali kupinga vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja mara baada ya baraza hilo kupitisha tamko hilo katika ukumbi wa AmabilisCentre mkoani Morogoro, kulia ni Katibu Mkuu Mtendaji wa Baraza hilo, Askofu David Mwasota.

BARAZA la maaskofu wa Kipentekoste Tanzania (PCT) limeungana na serikali kupinga vitendo vya ushoga na ndoa za jinsia moja na kudai kuwa vitendo hivyo endapo vitakubaliwa vitasababisha kuporomoka zaidi kwa maadili na kinyume na utamaduni wa kitanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Amabilis uliopo Mjini Morogoro, Mwenyekiti wa baraza hilo, Askofu David Batenzi alisema kuwa baraza hilo la maaskaofu limeungana na serikali katika kupinga ushoga na ndoa za jinsia moja ambao ni utamaduni mpya nchi unaotaka kukubali kutumika katika jamii ya kitanzania na kubainisha kuwa endapo vitendo hivyo vitakubalika vitachangia kuporomosha maadili na utamaduni wa kitanzania na afrika kwa ujumla.

Batenzi alisema kuwa viongozi wa serikali kukataa ushoga na ndoa za jinsia moja ni jambo sahihi kwani hilo ni kinyume na maadili na dini kuu za uislam na ukristo hivyo tabia hiyo ni tabia za mataifa ya maghalibi ambazo haziendani na tabia za dini zilizopo hapa nchini.

Alisema kuwa licha ya vitendo hivyo kuwa kinyume na mila za kiafrika pia zitasababisha kuikosesha nchi ya Tanzania Baraka kutokana na kuwa ushoga na ndoa za aina moja ni kinyume na uumbaji wa mungu amabpo kwa ujumla vitendo hivyo ni sawa na kukubali laana ndani ya nchi ya Tanzania.

Akinuuku maneno kutoka katika biblia kupitia wakoritho 6: 9- 10 alisema kuwa mungu aliziangamiza sodoma na gomola kwa moto kutokana na kuendesha vitendo vya ushoga na kubainisha kuwa waasherati wote hawataurithi ufalme wa mbingu.

“ushoga na ndoa za jinsia moja ni upotevu wa fikra ikiwemo ujinga na giza la moyo na kuwa endapo serikali ingekubali jambo hilo lingekuwa ni sawa na kuwavunjia heshima watanzania wenye tabia njema” alisema Batenzi.

Alisema kuwa amri za mungu na maandiko ya biblia ushoga na ndoa za jinsia moja ni laana kwa taifa na jamii ya watu wenye maadili mema kwani kutokana na kubadilisha maandiko ya biblia na kuhalalisha uchafu huo.

Tamko hilo lilitolewa mara baada ya kumalizika kwa semina ya kiroho ya siku tatu iliyowakutanisha maaskofu wa umoja wa makanisa ya Kipentekoste Tanzania (PCT) 48.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: