Raia 39 Somalia wauawa katika hujuma zinazodaiwa kuwa ni Marekani
Watu wasiopungua 39 wameuwa nchini Somalia baada ya ndege zisizo na rubani zinazo daiwakuwa kuwa ni nchi ya Marekani kushambulia kusini mwa nchini hiyo karibu na pwani ya Bahari ya Hindi.
Vilevile makumi ya watu pia wamejeruhiwa katika mashambulizi hayo.
Mashambulizi hayo yamelenga nje kidogo ya mji wa Kismayo ambao ni bandari muhimu ya Somalia ambako pia kunahesabiwa kuwa ngome ya waasi wa as Shabab.
Marekani imekuwa ikitumia ndege hizo zisizo na rubani kushambulia maeneo mbalimbali katika nchi za Afghanistan, Yemen, Pakistan, Iraq na Libya kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
Mashambulizi hayo yanafanywa na jeshi la Marekani katika nchi hizo kinyume cha sheria za kimataifa.
0 comments:
Post a Comment