BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

SH 159.2MILIONI ZATUMIKA KATIKA SIKUKUU YA EDD EL HAJI KUNUNUA KITOWEO MORO.


WALEMAVU WAKISHIRIKI MBIO KWA KUSHINDANA KATIKA BAISKELI YA MAGURUDUMU MATATU KWENYE UWANJA WA JAMHURI MOROGORO.

PICHA NA HABARI ENDELEA KUSHUKA CHINI.

JUMLA ya Sh159.2 milioni zimetolewa kwa ajili ya ununuzi wa ng’ombe, mbuzi na kondoo 1,570 walitumika kwa kitoweo katika sikukuu ya Edd-el-Haji kwa wakazi wa manispaa ya Morogoro.

Fedha hizi zilitolewa na taasisi nne za Darlber ya nchini Dubai, Eid Charity ya nchini Qatar, Friendship and Solidarity Trust (Rehema) na feza Schools za nchini Uturuki walitoa msaada wa fedha hizo na wafadhili wa ndani ili kuwawezesha wakazi wa Manispaa hiyo kuweza kusherehekea sikukuu hiyo.

Wakizungumza na mwandihsi wa habari hizi kwa nyakati tofauti mjini hapa Waratibu wa taasisi hizo walisema kuwa kati ya fedha hizo Sh 119.2milioni zilitolewa na wahisani wa ndani huku kiasi kingine kikitolewa na taasisi hizo.

Kiasi cha fedha cha sh 159.2Milioni kimetolewa na wafadhili wa ndani na nje Darlber ya nchini Dubai na Eid Charity ya nchini Qatar chini ya usimamizi wa taasisi ya Islamic Faoundatio Morogoro kwa ajili ya ununuzi wa wanyama 1570 ikiwa ni sehemu ya kutekeleza ibada ya kuchinja inayofanyika mara baada ya sala ya Edd El Haji kwa waumini wa dini ya kiislm.

Akizungumza na gazeti hili katika ofisi za taasisi ya Islamic Foundation Morogoro imamu mkuu wa msikiti wa Haki uliopo mtaa wa Karume, Ibrahim Twaha alisema kuwa kiasi kilichotolewa na wahisani wa ndani cha sh 159.2 Milioni kilitumika kununua mbuzi na kondoo kwa ajili ya kitoweo.

Twaha alisema kuwa taasisi hiyo ya Islamic Foundation Morogoro iliweza kugawa sehemu ya kitoweo hicho katika mikoa 11 mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani lengo likiwa kuwapa fulsa waumini wasiojiweza wa dini ya kiislam kuweza kusherekea sikukuu ya Edd El Haji.

Naye Siraj Jaffari alisema kuwa taasisi mbili kutoka nchini Uturuki za Friendship and Solidarity Trust (Rehema) na feza Schools walitoa msaada wa fedha kiasi cha sh 40Milioni ambazo zilitumika kununua ng’ombe 80 ambao walichinjwa na kugawa kwa waumini kupitia misikiti 20 iliyopo ndani ya Manispaa ya Morogoro.

Jaffari alisema kuwa mgao huo wa kitoweo hicho ulitolewa katika misikiti 20, shule ya sekondari ya Easternre, Chuo kikuu cha kiislam Morogoro na kituo cha Wazee cha Fungafunga ambapo makundi hayo yana mahitaji maalum huku baadhi ya makundi hayo yakiwa ni maskini.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: