Baadhi ya waandishi wa habari na walimu wa shule ya msingi Mazimbu A kata ya Mazimbu mkoani Morogoro wakiangalia sehemu ya kuogea inayotumiwa na mwalimu wa darasa la kwanza katika, Renfrida Mweji (59) ikiwa imezungushiwa mabati yaliyoshikiwa na mbao mkoani hapa.
Mwalimu wa darasa la kwanza shule ya msingi Mazimbu A kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro, Renfrida Mweji (59) akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) choo kinachomilikiwa na shule hiyo namna kilivyobomoka huku akiwa ameweka mbao na gogo ili kuziba sehemu ambayo imebomoka na kuweza kutumia mkoani hapa.
SHULE ya msingi Mazimbu A iliyopo kata ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro imetenga kiasi cha sh 252Milioni kwa ajili ya kupunguza kero mbalimbali ikiwemo shule hiyo kukosa vyoo kwa matumizi ya wanafunzi na walimu kwa miaka 17 mkoani hapa.
Kuibuka kwa kero hiyo ya shule ya msingi Mazimbu A kukosa matundu vya vyoo kwa muda wa miaka 17 imetokana na kuwepo kwa kero ya kubomoka kwa shimo la choo katika nyumba anayoishi mwalimu wa darasa la kwanza shule hiyo, Renfrida Mweji (59) huku likitumika kwa zaidi ya mwaka mmoja.
Akizungumza na waandishi wa habari ofosini kwake Afisa Mtendaji wa kata ya Mazimbu mkoani hapa, Winfreda Chausi alisema kata ya Mazimbu ina mpango wa kutumia kiasi cha sh 254Milioni kwa ajili ya kupunguza baadhi ya kero mbalimbali zinaikabili shule ya msingi Mazimbu A Manispaa ya Morogoro ikiwemo kukamilisha ujenzi wa matundu 12 kati ya 58 yanayohitajika baada ya shule hiyo kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya haja kubwa na ndogo kwa wanafunzi na walimu kwa miaka 17.
Chausi alisema oktoba 17 mwaka huu baraza la maendeleo la kata ya Mazimbu ilifanya ziara katika shule hiyo lengo likiwa kuziibua changamoto mbalimbali ikiwemo za uhaba wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia vitabu, chaki na manila, uhaba wa majengo ya shule, ushirikiano mdogo kati ya walimu na wazazi.
Changamoto nyingine ni shule kukosa uzio unaowapa mwanza wakazi kupita eneo la shule na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wanafunzi wakati vipindi vya masomo vikiendelea na shule kukosa vyoo hali ambayo huwalazimu walimu na wanafunzi kutumia vyoo vya shule ya msingi Mazimbu B na kusababisha msongomano mkubwa kwa wanafunzi wakati wa kwenda haja.
“tulifanya ziara ya kutembelea shule ya msingi Mazimbu A kwa lengo la kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili lakini katika shule ziara hiyo kero zimekuwa nyingi hivyo baraza la maendeleo la kata limeanzimia kutatua kero ya vyoo kwa kumalizia ujenzi wa matundu 12 ili kupunguza msongomano kwa wanafunzi hao” alisema Chausi.
Mpango huo ukikamilika hasa baada ya kupanga kutumia kiasi cha sh 254milioni itasaidia kujenga vyumba vya madarasa mapya 19 kutoka na kuwepo kwa madarasa nane yanayotumiwa hivi sasa, ofisi za walimu mbili, stoo moja maktba na nyumba za walimu moja. Alisema Chausi.
Aidha akizungumzia juu ya choo kibovu kinachotumiwa na mwalimu wa darasa la kwanza shule hiyo, Renfrida Mweji (59) alisema wanatarajia kuitisha kikao cha wazazi ili kujadili namna ya kujenga choo cha mwalimu huyo.
Naye mwalimu wa darasa la kwanza shule ya msingi Mazimbu A, Renfrida Mweji akizungumza na mwandishi wa habari hizi alisema kuwa choo hicho amekuwa akitumia kwa mwaka mmoja sasa licha kutoa taarifa katika ngazi husika hivyo hulazimika kutumia mbinu mbalimbali wakati kuingia kwa ajili ya haja kubwa kutokana na sehemu kubwa ya choo hicho kuweka mbao na gogo linalofanya kupata nafasi ya kuingia katika choo hicho.
Mweji alisema kuwa Amekuwa akiishi kwa wasiwasi kutokana na kuishi na mlemavu wa macho asiyeona na mzee asiyejiweza hivyo humlazimu kufika mara kwa mara nyumbani hapo kwa ajili ya kuangalia usalama wao huku akidai hali hiyo inatokona na mmoja wa ndugu zake kutumbukia mguu ndani ya choo hicho wakati akielekea kwenye choo kwa ajili ya haja kabla ya watu waliokuwa karibu kutoa msaada wa kumnasua.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / SHULE YA MSINGI MAZIMBU A MORO YATENGEWA SH 252MILIONI ILI KUPUNGUZA KERO MBALIMBALI IKIWEMO YA KUKOSA VYOO KWA MIAKA 17.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment