Viongozi wa IGAD wakutana kujadilia al-Shabab
Wapiganaji wa Al-Shabab.
Viongozi wa nchi sita za kiafrika watakutana hii leo Ijumaa kuzungumzia mikakati ya kuimarisha kampeni ya kijeshi inayolenga kulimaliza kundi la wanamgambo wa Al- shabab nchini Somalia.
Viongozi hao wanatazamia kupata uungaji mkono wa Umoja Mataifa kama kiungo muhimu katika juhudi za kuvunja ngome za Al-shabab kwenye maeneo yaliyokumbwa na njaa kusini na katikati ya Somalia.
Aidha viongozi wa Jumuiya ya mamlaka na maendeleo ya serikali katika ukanda wa Afrika Mashariki -IGAD, , wanakutana mji mkuu wa Ethiopia wakiwa na matumaini ya kuongeza mashambulizi dhidi ya al-Shabab nchini Somalia.
Wanatazamia vikosi Umoja wa Afrika - AMISOM vitaendelea kudhibiti mji mkuu Mogadishu. Kuwasili kwa vikosi zaidi, pamoja na ushirikiano wa wanamgambo kutoka koo mbalimbali za Somalia, kadhalika vikosi vya serikali ya mpito, kunatarajiwa kuipa fursa serikali ya Somalia kupanuwa udhibiti wa maeneo zaidi nchini humo.
Vikosi vya Kenya huko kusini mwa Somalia vyasemekana kutopata ufanisi mkubwa kupitia kampeni yao, ambayo imekuwa ikiendelea kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa, na ambayo imehujumiwa na hali mbaya ya hali ya hewa, na changamoto nyingine.
0 comments:
Post a Comment