BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

RAIS WA ZAMANI WA JAMHURI YA UCZECH, VACLAV HAVEL (75) AFARIKI DUNIA .


VACLAV HAVEL (75) mwandishi wa tamthilia aliyekuja kuwa rais wa kwanza wa Czechoslovakia, baada ya ukoministi, amefariki.

Rais huyo wa zamani amekuwa akiugua kwa miaka kadha, na mwaka wake wa mwisho, amekuwa akipumzika kwenye nyumba yake ya shamba.

Mwaka wa 1989 Vaclav Havel alikuwa mwandishi wa tamthilia aliyezungumza kwa upole, ambaye alifungwa kwa sababu ya msimamo wake wa kutetea demokrasia na sheria.

Alikuwa hajulikani na wengi, lakini katika majuma machache waandamanaji waliokusanyika kupinga ukoministi walianza kutaja jina lake kwa kelele.

Na Disemba mwaka wa 1989, jambo ambalo hata halikufikiria lilitokea - mwandishi huyo akawa rais wa Czechoslovakia.

Miaka mitatu baadae alishuhudia nchi yake ikigawika pande mbili - Czech na Slovakia - jambo ambalo hajakubaliana nalo, na lilimuumiza sana.

Lakini aligombea urais tena katika Jamhuri ya Czech huru, na aliongoza nchi hadi mwaka 2003.

Baada ya kustaafu alikuwa akitunga tamthilia, na mwaka jana alifanikiwa kupata ndoto yake..kwa kuwa mkurugenzi (director) wa tamthilia yake ya karibuni kabisa.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: