BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

TUNASAKA MSHINDI WA TATU MCHEZO WA KIKAPU SHIMIVUTA 2011.


MCHEZA WA TIMU YA KIKAPU YA CHUO CHA USIMAMIZI WA FEDHA (IFM) AKIJARIBU KUWATOKA WACHEZAJI WA CHUO CHA UHASIBU TANZANIA (TIA) WAKATI WA MCHEZO WA KUTAFUTA MSHINDI WA TATU WA MCHEZO WA KIKAPU MASHINDANO HAYO YA SHIMIVUTA KWENUE UWANJA WA BWALO LA UMWEMA LA JKT MJINI MOROGORO AMBAPO KATIKA MCHEZO HUO TIA ILISHINDA KWA VIKAPU 43-42.


CHUO cha elimu ya biashara (CBE) kimefanikiwa kutwaamakombe matatu tofauti kwa kushika nafasi ya kwanza baada ya kufanya vizuri michezoyao ya fainali katika mashindano ya shirikisho la michezo kwa vyuo vya elimu yajuu mchanganyiko Tanzania (SHIMIVUTA) kwa mwaka 2011/2012 yamemalizika jana kwenyeuwanja wa jamhuri mkoani Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili mkoani hapa Waziri wa Michezowa chuo hicho, Shaibu Twalib alisema chuo chao kimefanikiwa kutwaa ubingwa wamatatu kwa michezo ya soka, netiboli na kikapu kwa mwaka 2011/2012 baada ya kuingizatimu tatu katika fainali ya mashindano hayo.

Twalibu alisema CBE ilifanikiwa kuingiza timu tatu katikafainali kwa michezo ya soka, netiboli na kikapu na kufanikiwa kushinda yotejambo ambalo limeleta furaha ndani ya chuo hicho.

“tumefanikiwa kutwaa vikombe vitatu ya shimivuta kwamwaka 2011/2012 mimi kama waziri wa michezo jambo hili nimelifurahisha sanalakini nawapongeza wachezaji wote wa michezo wote walioshiriki katika mashindanohayo kwa kuonyesha kwa moyo mmoja hadi tumefanikiwa kutwaa vikombe hivyo”. AlisemaTwalibu.

Twalibu alisema katika fainali za mashindano hayompira wa kikapu ndio uliokuwa na ushindani mkubwa sana hasa baada ya kuilaza kwashida timu ya chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini kwa vikapu 40-39 huku kwaupande wa mchezo wa netiboli waliitandika timu ya chuo cha serikali za mitaa (LGTI)kwa idadi ya bao 38-30.

Mchezo wa soka timu yao haikuweza kupata ushindani mkalikutokana na wachezaji kuwadhibiti wachezaji wa timu ya chuo cha serikali zamitaa (LGTI) kufuatia kuitandika katika mchezo wa fainali kwa bao 5-0.

Naye Katibu Mkuu wa Shimivuta, Augustine Matemalisema katika mashindano ya mwaka huu timu za chuo cha biashara (CBE) imefanikiwakutwaa makombe matatu ya michezo ya soka, netiboli na kikapu baada ya kuingizahizo katika fainali.

Matem alisema kuwa mashindano ya mwaka 2011 yamekuwana mafanikio makubwa baada ya vyuo 14 kushiriki katika mashindano hayo tofautina miaka iliyopita ambapo vyuo 11 hadi 12 ndio waliokuwa wakishiriki mashindanohayo.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: