BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MKAZI WA CHANIKA AOMBA MSAADA WA MIKONO YA BANDIA KWA WASAMALIA WEMA MORO.


MKAZI wa kijiji cha Chanika iliyopo Jijini Dar es Salaam, Ally Habibu (30) anahitaji msaada wa kiasi cha sh1.9Milioni kwa ajili ya kumsaidia kununua mikono ya bandia sambamba na kupatiwa kiasi cha fedha ambacho kitasaidi kuanzisha mradi ya kufanya biashara ili kuweza kupata fedha za kujiku na maisha.

Akizungumza na BLOGU hili mkoani Morogoro, Habibu ameelekeza ombi hilo kwa serikali, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na taasisi za dini ili kumsaidia upatikanaji wa mikono hiyo kutokana na familia yake kushindwa kumudu ghalama zake za kununua mikono hiyo ya bandia.

Tukio hilo ambalo alilipata baada ya kuvamiwa na majambazi mwaka 2009 ambapo walimkamata na kuanza kumcharanga panga hali iliyopelekea mikono yake miwili kugawanyika vipande viwili wakati akienda kununua bidhaa za genge majira ya saa 12 asubuhi katika eneo la Chanika.

Habibu alisema kiasi hicho cha fedha ni kwa ajili ya ununuzi wa mikono bandia ambayo itamsaidia kwa kiasi kikubwa kumudu kuwahudumia wateja wake mara baada ya kuanzisha mradi wo wote utakaomsaidia kujikimu na hali ngumu ya kimaisha.

Aliwaomba wananchi pamoja na mashirika hayo kumsaidia ili aweze kufanya kazi na kwamba ikiwa atapata mikono hiyo ya bandia ni rahisi kufanya kazi ndogo ndogo tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo hana uwezo wa kufanya kazi yeyote.

Habubu alisema kuwa kiasi hicho cha fedha kitatumika kwa ajili ya kupata mikono hiyo aliambiwa katika hospitali ya KCMC Moshi mkoani Kilimanjaro mwaka 2009 alikokwenda kupatiwa matibabu zaidi na kwamba alishindwa kupata huduma hiyo kutokana na kukosa fedha.

Akielezea zaidi juu ya tukio hilo alisema kuwa akiwa njiani kutokea Chanika kuelekea shambani katika eneo ka Kise kwa ajili ya kununua bidhaa za gengeni alikutana na kijana aliyemuomba amsaidie kufika katika eneo la Kise kwa mzee mmoja aliyemtaja kwa jina la Azizi huku yeye akiwa na baiskeli.

Alisema kuwa katika mkasi huo alimpa alimsaidi kijana huyo katika baiskeli yake kwa kumpakiza nyumba ghafla kijana huyo alitoa panga na kuanza kumjeruhi sehemu mbalimbali za mwili wake ikiwemo kichwani na mikononi na hivyo kumsababishia majeraha makubwa mwilini ambapo alilazimika kukatwa mikono yote miwili katika hospitalini.

Tangu kupatwa na ulemavu huo amekuwa akiishi maisha ya shida na hivyo kulazimika kuishi maisha ya kuombaomba kutokana na familia yake kutokuwa na uwezo wa kumsaidia huku yeye akiwa na familia ya mke na watoto wawili wanaomtegemea.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: