Kwa ufupi
Hata hivyo, hoja hiyo ilizimwa na Ndugai, ambaye
baadaye aliruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne
Maghembe, hatua ambayo iliwafanya wabunge wote.
KITENDO
cha kuzitupa hoja zilizowasilishwa bungeni na wabunge John Mnyika wa
Chadema na James Mbatia wa NCCR-Mageuzi, kimesababisha chama kikuu cha
upinzani Chadema, kuamua kufanya maandamano nchi nzima ili kuwashtaki
kwa wananchi Spika wa Bunge, Anne Makinda na Naibu wake Job Ndugai.
Hata hivyo, hoja hiyo ilizimwa na Ndugai, ambaye baadaye aliruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, hatua ambayo iliwafanya wabunge wote wa upinzani kusimama kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua hiyo ya Ndugai wakidai kwamba Naibu Spika huyo amevunja kanuni alizopaswa kuzisimamia.
Sambamba na tukio hilo Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliwasilisha hoja binafsi akidai Serikali haina mitalaa ya elimu na kutaka Bunge kuunda kamati teule kuchunguza udhaifu huo.
Naibu Spika Job Ndugai.
Maandamano hayo yatatanguliwa na mkutano wa
hadhara utakaofanyika kesho Viwanja vya Temeke Mwisho, Dar es Salaam,
sanjari na kuwapokea wabunge wake wanaorejea kutoka kwenye mkutano wa
Bunge uliomalizika jana Dododma.
Chadema kimedai kuwa kanuni za bunge zina
upungufu na kwamba kitendo cha spika na naibu wake kuzima hoja za
wabunge hao kinadhihirisha kuwa viongozi hao wa mhimili huo wa taifa
wameshindwa kulinda hoja zenye maslahi kwa wananchi na wameligeuza bunge
kuwa ‘kijiwe cha CCM’.
Hoja zilivyozimwa
Wiki hii, katika kikao hicho cha Bunge, Mnyika aliwasilisha hoja binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Wiki hii, katika kikao hicho cha Bunge, Mnyika aliwasilisha hoja binafsi akilitaka Bunge liazimie kuitaka Serikali ichukue hatua za haraka kuboresha upatikanaji wa majisafi na ushughulikiaji wa majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, hoja hiyo ilizimwa na Ndugai, ambaye baadaye aliruhusu kujadiliwa kwa hoja ya Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghembe, hatua ambayo iliwafanya wabunge wote wa upinzani kusimama kwa pamoja na kuanza kupiga kelele za kupinga hatua hiyo ya Ndugai wakidai kwamba Naibu Spika huyo amevunja kanuni alizopaswa kuzisimamia.
Kitendo hicho pia kilisababisha kikao
kuahirishwa kabla ya muda uliopangwa, huku hoja ya Profesa Maghembe ya
kupendekeza kuondolewa bungeni kwa hoja ya Mnyika ikiungwa mkono na
wabunge wa CCM.
Sambamba na tukio hilo Mbunge wa kuteuliwa, James Mbatia aliwasilisha hoja binafsi akidai Serikali haina mitalaa ya elimu na kutaka Bunge kuunda kamati teule kuchunguza udhaifu huo.
Hata hivyo, hoja hiyo ilitupiliwa mbali,
badala yake Ndugai aliunda kamati kuichunguza mitalaa hiyo kuangalia
uhalali wake, kabla ya kuthibitishwa na Bunge.
Licha ya kuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kuwasilisha bungeni mitalaa hiyo juzi,
ambapo Mbatia alisema hakubaliani na mitalaa hiyo kwa maelezo kuwa
kilichowasilishwa siyo kilichoahidiwa awali na Dk Kawambwa.
Tamko la Chadema.
Katika tamko la jana la Chadema mbele ya waandishi wa habari jana, Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Organaizesheni na Mafunzo wa chama hicho, Benson Kigaira alisema:
“Kwanza tutawapokea wabunge wote wa upinzani pale Ubungo na baadaye yataanza maandamano kuanzia eneo la Tazara, hadi katika Viwanja vya Temeke Mwisho, ambako utafanyika mkutano mkubwa wa hadhara.”

Akizungumzia kibali cha Jeshi la Polisi,
Kigaira alisema tayari wameshatoa taarifa, uwanja wanaotarajia kufanya
mkutano huo siku ya Jumapili hautakuwa na shughuli nyingine, hivyo
hakuna kisingizio chochote wala sababu za kuzuiliwa kwa mkutano na
maandamano hayo.
Alisema kilichofanywa na viongozi hao wakuu wa
Bunge, huku Serikali ikiwataka wananchi kuamini kuwa wabunge wa Chadema
ni wakorofi ni sawa na ‘’kubaka demokrasia na ubabe wa kiti cha
Spika.’’
0 comments:
Post a Comment