BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MECHI YA DUNIA MANCHESTER UNITED NA REAL MADRID

Kwa ufupi:
“Isipite sekunde mtu huyu kuwa huru. Ni mjanja, siyo lazima mpira umfuate, anaweza kwenda upande wowote na kufunga,” alisema Neville.


WASHAMBULIAJI WANAOTARAJIWA KUPACHIKA MABAO KATIKA MCHEZO HUO.
 
WAKATI Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho akiufananisha mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Manchester United kuwa ni ‘Mechi ya Dunia’, nahodha wa zamani wa United, Gary Neville ameionya klabu hiyo kumchunga vilivyo mshambuliaji Cristiano Ronaldo.

Neville aliyecheza na Ronaldo Old Trafford mwaka 2003 mpaka 2009, amesema nyota huyo wa Ureno, ni kama ‘mnyama’ anayetafuta walinzi dhaifu.


Nahodha huyo aliyecheza mechi 602 akiwa United kabla ya kustaafu anasema United italazimika kumchunga Ronaldo kila sekunde ya mchezo.

“Isipite sekunde mtu huyu kuwa huru. Ni mjanja, siyo lazima mpira umfuate, anaweza kwenda upande wowote na kufunga,” alisema Neville.


Madrid inaingia uwanjani kupambana na United ikiwa safi na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sevilla Ligi Kuu Hispania.

Ronaldo (28) amefikisha ‘hat-trick’ 20 tangu alipojiunga Real Madrid, ambapo ya mwisho kabla ya mchezo wa leo ilikuwa ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Sevilla.


Pia ana rekodi ya kufunga mabao 182 katika mechi 179 alizocheza na mabingwa hao wa Hispania.

Neville anaamini kwa sasa mshambuliaji huyo wa Real Madrid ni bora zaidi kuliko wakati akicheza katika Uwanja wa Old Trafford.
“Hii ni mechi ngumu, mechi itakayotikisa dunia yote.

Kwa nini nilisema mechi ya dunia? Kila mtu anahitaji kuishuhudia,” alisema Mourinho.


“Ni mechi ya timu mbili zenye wachezaji bora duniani na makocha bora pia,” alisema kocha huyo wa zamani Porto, Chelsea na Inter Milan.

Aliongeza: “Kila mchezaji [United, Madrid] atataka kucheza, hakuna atakayefurahi kupumzishwa kwa maana hii ni mechi kubwa ya kushuhudiwa na dunia yote.”


Mourinho alikuwa Uwanja wa Old Trafford Jumapili iliyopita kuipeleleza United wakati ikicheza na Everton mechi ya Ligi Kuu England na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Bernabeu ni wa kwanza kwa Ronaldo dhidi ya timu yake ya zamani tangu alipoondoka kwa uhamisho ulioweka rekodi (Paundi 80 milioni) mwaka 2009.

Akiuelezea mchezo huo, Alex Ferguson alisema ni mechi ya kuweka urafiki pembeni. “Sifikirii kuwa na urafiki na mtu,” alisema Ferguson.


“Nawezaje kumwacha mpinzani wangu apite barabara ninayopita?” aliongeza.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: