MELI
ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC)
imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo
wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo
kwenye Meli hiyo.
Moto huo
uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na
kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo
katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika kadhaa na
kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
Kwa
mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao
hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa
wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa
wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo ndipo cheche
za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia
mizigo na kuanza kuwaka.
Sehemu
hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito
ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani
Kagera leo usiku.
Ni
hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa
magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa
kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
Maafisa
wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo
mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa
tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa
katika chumba cha kuhifadhia mizigo.Picha kwa Hisani ya G sengo Blog
Read more: http://audifacejackson.blogspot.com/#ixzz2KIOSFcKk
0 comments:
Post a Comment