|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi (wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria upokeaji wa magari maalumu ya kusafirishia chanjo kwa kuzingatia mnyororo badiri. Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt na Mbunge wa Temeke Abbas Mtemvu. Mbali na kupokea magari hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete, Dk. Mwinyi alifungua Jengo la Kisasa la ghala la kuhifadhi dawa katika Makao Makuu ya Bohari ya dawa Dar es Salaam leo. |
|
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (kulia),akimuelekeza jambo Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi (kushoto), juu ya ubora wa ghala jipya la kisasa la kuhifadhia dawa, baada ya kulizindua katika Makao Makuu ya Bohari ya Dawa (MSD), Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mbunge Viti maalunu Martha Mlata na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt. |
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Hussein Mwinyi, akikata utepe kuashiria kupokea madawa na vifaa tiba vilivyotolewa na Madaktari wa Afrika kwa Serikali. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Tiba wa Madaktari Afrika, Dk.Dilan Ellegale na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt. |
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Bohari ya madawa (waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu. |
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wawakilishi wa Shirika la Afya Duniani ( (waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid na Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu. |
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (wa tatu kushoto waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Afya ya Bunge (waliosimama nyuma). Kutoka kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Donan Mmbando, Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani, Mbunge wa Kigamboni Dk. Faustine Ndungululile, Mwakilishi Mkazi wa Shirika la kuhudumia watoto duniani (UNICEF), DK. Jama Gulaid |
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (hayupo pichani) akiwaongoza wageni waalikwa wakati akipokea magari mawili maalumu ya kusafirishia dawa. |
|
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Cosmas Mwaifwani (kulia), akiwaongoza Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi na Balozi wa Marekani nchini Alfonso Lenhardt, kwenda kuzindua magari maalumu ya kusafirishia dawa. |
|
Mfanyakazi wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha jinsi ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa kutumia toroli maalumu. |
|
Dereva wa Bohari ya Dawa (MSD), akionesha jinsi ya kubeba dawa ndani ya bohari hiyo kwa kutumia foku lifti. |
|
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hussein Mwinyi (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali kwenye hafla hiyo |
|
Wafanyakazi wa Bohari ya Madawa (MSD), wakiwa kwenye hafla hiyo |
Kaimu Mganga Mkuu wa Serikali Dk.Donan
Mmbando
akihutubia kwenye sherehe hiyo.
0 comments:
Post a Comment