TANZANIA
imepata tuzo tatu za maajabu saba ya Afrika kupitia vivutio vyake bora
vya utalii vya Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya
Serengeti ambayo ndio iliongoza kwa kupata kura nyingi kuliko nchi
nyingine yeyote.
Akitangaza
matokeo hayo jana mjini hapa rais wa taasisi iliyoandaa tuzo hiyo Dk.
Phillip Imler wa Marekani mbele ya waziri mkuu Mizengo Pinda alisema
sababu iliyopelekea Tanzania kupata ushindi huo ni kutokana na kuwa na
vivutio vya kipekee.
Akielezea
hifadhi ya taifa ya Serengeti alisema kuwa ndio hifadhi ya kipekee
iliyopata kura nyingi na kutokana na tabia za misafara ya wanyama
wanaohama kwa msimu maarufu kama annul animal migration.
WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, aliyekuwa mgeni rasmi katika ghafla hiyo, alisema
kuwa nchi za Afrika zina vivutio vingi vya utalii na fursa kubwa ya
kukuza pato kupitia utalii huo.
Alisema
kutokana na sifa ambayo Tanzania imezipata kupitia vivutio vyake vitatu
itaendelea kuvitunza kuhakikisha kuwa vinavutia zaidi watalii na
kuongeza pato la taifa.
“Afrika
ina vivutio vingi vyenye kuvutia hivyo kila nchi ni lazima ijivunie
rasilimali hizo kwa kuvitunza na kuviendeleza,”alisema
“Kwa
Tanzania ni bahati ya pekee kwa kuweza kupata tuzo tatu za maajabu saba
ya Afrika ambazo ni za Mlima Kilimanjaro, Bonde la Ngorongoro pamoja na
hifadhi ya Taifa ya Serengeti hivyo ni wajibu wa kuvitunza na
kuviendeleza,”alisema Pinda.
Aliongezea
kuwa iwapo watanzania wataendeleza tabia ya utunzaji wa vivutio
vilivyopo nchini, nchi itaendelea kupata sifa duniani kote.
Naye
Mkurugenzi wa Hifadhi za Taifa,(TANAPA),Dkt. Alan Kijazi alisema mlima
Kilimanjaro ni mlima mrefu barani Afrika na hivyo una kila sababu ya
kushinda na watanzania waendelee kuutunza.
Dkt
Kijazi alisema kuwa hifadhi hiyo imeshinda kwa kuwa kuwa na wanyama wa
kila aina kama Big Seven, Simba, tembo, Viboko, Nyati, Vifaru, Sokwe na
Mamba.
MBALI na Tanzania Dk. Imler alivitaja vivutio vingine vilivyoshinda kuwa ni
Red sea Reefs, Okavango Inland delta iliyopo nchini Botwasana, Sahara
Desert na River Nile.
Aidha
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamis Kagasheki alisema ushindi
huo ni historia kubwa duniani na kwamba ni jambo la watanzania wote
kujivunia.
Pia aliwashukuru wananchi walioshiriki katika mchakato mzima wa kupiga kura na kuviwezesha kuingia katika ushindi kwa mara tatu.
0 comments:
Post a Comment