BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM, CHADEMA DAR WAMGEUZIA KIBAO DK KIKWETE.

Kwa ufupi
Wafuasi wa Chadema waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa Chadema, kupiga kelele juu ya suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.  
http://www.mwananchi.co.tz
RAIS KIKWETE.
Dar es Salaam.
NI nadra kutokea lakini wafuasi wa vyama vya siasa vya CCM na Chadema, wameungana kumweleza Rais Jakaya Kikwete kuhusu kero ya maji eneo la Kimara-Golani, Dar es Salaam.
Rais Kikwete alikutana na hali hiyo wakati akifungua Daraja la Kimara jana, tukio hilo liliwakusanya watu wengi hasa wanachama wa CCM na Chadema waliokuwa wamevalia sare za vyama vyao.

Wafuasi wa Chadema waliongozwa na Mbunge wa Ubungo, John Mnyika ambao walikuwa wakipeperusha bendera za chama chao na kuimba nyimbo mbalimbali huku wakidai maji. 


Hata hivyo, kutokana na hali hiyo, wafuasi wa CCM waliungana na wenzao wa Chadema, kupiga kelele juu ya suala hilo kiasi cha kugusa hisia za Rais Kikwete.

Akizungumza baada ya uzinduzi wa daraja hilo, Rais Kikwete aliahidi kuitisha kikao Jumatatu ijayo kitakachomhusisha Profesa Maghembe na maofisa wa wizara yake, wabunge wa Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa, wakuu wa wilaya ili kuweka mikatati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hilo.

“Ninaomba Machi 25... tukutane ili tuweke mikakati ya pamoja kutafuta ufumbuzi wa suala hili,” alisema Rais Kikwete.

Akiwa Hospitali ya Mwananyamala, Rais Kikwete alizindua maabara ya kisasa kwa ajili ya uchunguzi na akazungumzia suala la dawa za kulevya kwa kusema atahakikisha mapambano yanaendelea kwani dawa hizo zinaua nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: