BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAFURIKO YAATHIRI MAKAZI YA WATU JIJINI DAR ES SALAAM



 


http://www.mtanzania.co.tz
 BAADHI ya maeneo ya Jiji la Dar es Salaam, jana yalikumbwa na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa ilionyesha jana asubuhi. 

Mafuriko hayo yaliathiri baadhi ya makazi ya wananchi kwa kuwa maji yalijaa katika nyumba zao.

Katika Barabara ya Mandela maeneo ya Tabata jirani na ofisi za Gazeti la Mwananchi, maji yalijaa barabarani na kusababisha usumbufu wa magari na waenda kwa miguu.

Kwenye maeneo hayo, magari yalikuwa yakiendeshwa kwa mwendo wa taratibu na wakati mwingine yalikuwa yakisimama kwa vile madereva walishindwa kukabiliana na kasi ya maji hayo.

Pamoja na hayo, hali ilionekana kuwa mbaya zaidi katika maeneo ya Ubungo Darajani ambako maji yalikuwa yamefurika na kukaribia juu ya daraja.

Wakati maji hayo yakipita, baadhi ya mali zikiwamo magodoro, vyombo vya ndani na samani nyingine, vilikuwa vikielea juu ya maji.

Kutokana na hali hiyo, wananchi walijaa darajani hapo wakishuhudia mafuriko hayo na wengine wakipiga kelele kila walipokuwa wakiona mali zikielea.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: