BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

DOWANS KAA LA MOTO, MAHAKAMA YA FURANI YAIAMURU TENESCO KUILIPA DOWANS FIDIA.

Kwa ufupi.
“Walifanya haraka kuvunja mkataba wakati ilikuwa imebaki miezi mitatu tu uishe. Kulikuwa na wanasiasa na wataalamu wetu walioshinikiza mkataba uvunjwe na hayo ndiyo matokeo yake,” alisema Keissy.

Uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani walikubaliana na hoja za pingamizi la Wakili wa Dowans, Kennedy Fungamtama, kuwa maombi hayo yaliwasilishwa nje ya muda.
http://www.mwananchi.co.tz
DAR ES SALAAM. 
KUFUATIA Mahakama ya Rufani kutupilia mbali maombi ya Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) kuzuia utekelezaji wa hukumu ya Mahakama Kuu iliyoliamuru liilipe fidia Kampuni ya Kufua Umeme wa Dharura, Dowans, wananchi wamehoji sababu ya Serikali kuzembea hadi deni hilo kuongezeka.
Tanesco iliwasilisha katika Mahakama ya Rufani maombi ya kusimamisha utekelezwaji wa hukumu ya Mahakama Kuu, ikidai kuwa Dola za Marekani 65 milioni, walizoamriwa na ICC kuilipa Dowans ni kiasi kikubwa, endapo kitalipwa Tanesco itapata hasara kiuchumi.
Tanesco iliongeza kuwa kama mchakato wa utekelezaji wa hukumu hiyo utaendelea, utaathiri uwezo wake wa kuzalisha na kusambaza umeme nchini na hivyo kusababisha tatizo kubwa la ukosefu wa umeme, ambao utaathiri uchumi wa nchi kwa jumla.
Hata hivyo, wakati hukumu ya sasa inatolewa riba ya deni hilo imeongezeka hadi kufikia dola 122 milioni ikiwa ni ongezeko la dola 58 milioni.

Wakizungumzia ongezeko hilo baadhi ya wanasiasa wameilaumu Serikali kwa kuzembea hadi deni hilo  kufikia kiasi hicho.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ally Keissy alisema kuwa hasara hiyo inatokana na wanasiasa na wataalamu wa Serikali kulazimisha kuvunjwa kwa mkataba wa Dowans badala ya kusubiri muda wake uishe.
“Walifanya haraka kuvunja mkataba wakati ilikuwa imebaki miezi mitatu tu uishe. Kulikuwa na wanasiasa na wataalamu wetu walioshinikiza mkataba uvunjwe na hayo ndiyo matokeo yake,” alisema Keissy.
Naye Mbunge wa kuteuliwa na Mwenyekiti wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia ameilaumu Serikali kwa kutokuwa makini inapoingia mikataba.
“Mambo ya mikataba ni ya kisheria kati ya pande mbili. Lazima kuwe na umakini, kwanza ujue nia ya kuingia mkataba, matazamio na faida zake. Lazima pia kuwe na elimu kwa wataalamu wetu,” alisema Mbatia na kuongeza;
“Hapa Serikali imekosa umakini ndiyo maana tumeingia kwenye hasara kama hiyo. Kwa sasa siwezi kusema hatua gani ichukuliwe kwa sababu sijaiona hukumu lakini huo ni uzembe.”

Naye Mbunge wa Lindi Mjini, Salum Barwany alisema hayo ndiyo matokeo ya Serikali kutokuwa makini na mikataba.

“Sisi kama wabunge tuliipigia mno kelele Serikali bungeni na hata Mwenyekiti wetu wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alishasema, hakutakuwa na mafanikio hata kama itakata rufaa. Sasa ndiyo yametokea. Sasa huu ni mzigo watakaobebeshwa wananchi,” alisema Barwany na kuongeza:

“Kama wabunge tunapendekeza kuwa mikataba kama hiyo ifikishwe bungeni ili tuijadili kuliko kuwaachia tu watalaamu.”

Kwa upande wake wakili na mwanaharakati wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia alisema kuwa makosa yalikwishafanyika tangu mwanzo hivyo, Serikali iwawajibishe walioingia mkataba huo au hata kushauri.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: