BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

CCM YAIBWAGA CHADEMA SUMBWANGA

Aeshi Hilary.YamseboAliekuwa mgombea wa CHADEMA, Mwalimu Norbet Yamsebo akiwa na furaha mara baada ya kuibuka mshindi
Mahakama Kuu Kanda ya Sumbawanga kutengua matokeo ya ubunge wa jimbo la Sumbawanga mjini yaliyompa ushindi mgombea wake Aeshi Hilal. http://www.freemedia.co.tz

MAHAKAMA ya Rufani Tanzania imerejesha ubunge wa Sumbawanga Mjini kwa Aeshi Hilary (CCM) uliotenguliwa na Mahakama Kuu kanda ya Sumbawanga kwenye kesi ya kupinga uhalali wa matokeo yaliyompa ushindi mbunge huyo.

Hukumu ya rufani hiyo ilisomwa Dar es Salaam jana na Naibu Msajili wa Mahakama Zahara Maruma na kueleza kuwa sababu zilizotumika kutengua ubunge huo hazikuthibitika.

Aeshi alichaguliwa kuwa mbunge wa Sumbawanga mjini wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 baada ya kuwashinda wagombea wengine akiwemo Norbet Yamsebo (CHADEMA) ambaye alifungua kesi kupinga matokeo hayo.

Naibu msajili huyo alizitaja sababu hizo kuwa ni vurugu wakati wa kampeni zilizosababisha Yamsebo kushindwa kufanya mikutano yake na madai ya rushwa iliyotolewa na mawakala wa Aeshi kwenye shule ya msingi Kantalamba Mazoezini.

Akisoma hukumu hiyo, Naibu Msajili alisema kulikuwa na mkanganyiko kwenye ushahidi uliotolewa Mahakama Kuu ambapo mashahidi walishindwa kuonyesha namna vurugu hizo zilivyoathiri matokeo ya uchaguzi.

Kuhusu madai ya rushwa Mahakama ya Rufani imetilia shaka ushahidi uliotolewa na mtu mmoja aliyedai kwamba aliwaona mawakala wa Aeshi wakitoa fedha huku akishindwa kuthibitisha madai hayo.

Awali Aeshi alikata rufani kupinga hukumu ya kutenguliwa kwa ubunge wake iliyosomwa Aprili 30, 2013 na aliyekua Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Sumba
wanga, Bethuel Mmmila.

Hukumu hiyo iliyoandaliwa na jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Edward Rutakangwa, Profesa Ibrahim Juma na Dk. Steven Bwana.

Baada ya hukumu hiyo waliokuwa walalamikiwa Aeshi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) walikata rufani kupinga hukumu hiyo ambapo mahakama ya rufani ilizisikiliza Aprili 19 mwaka huu.

Mawakili wa Serikali Michael Luena na Karim Rashid kwa niaba ya AG waliwasilisha hoja 10 za kupinga uamuzi wa hukumu ya Mahakama Kuu kwa vile kulikuwa na dosari za kisheria.

Akizungumza nje ya mahakama baada ya uamuzi huo Yamsebo aliwataka wananchi wa Sumbawanga mjini watulie huku akibainisha kwamba atakwenda kuzungumza na viongozi wake ili kujua iwapo atakata rufani kupinga uamuzi huo.

“Mahakama imeamua tofauti na matarajio yangu kwa sasa sina la kusema kama nitapinga… hii ni kama harusi lazima nishirikiane na viongozi kujua, nasubiri nitakapokutana nao nitasema neno,” alisema Yamsebo.

Naye Aeshi alisema mahakama imetenda haki na kwamba anarudi jimboni kuwatumikia wananchi huku akisisitiza kwamba shughuli za maendeleo zilizosimama wakati wa kesi hii zitaendelea kwa nguvu, kasi na ari zaidi.

“Namshukuru Mwenyezi Mungu, mahakama imetenda haki na imeonekana… nawaomba wapigakura wa Sumbawanga Mjini wajiandae kwa sababu nakwenda kutekeleza ahadi kwa vitendo,” alisema Aeshi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: