Kwa ufupi
Shambulio hilo lilitokea wakati balozi huyo akiwa
amesimama na mwenyeji wake, Askofu Mkuu, Josephat Lebulu, mapadri na
watawa kutoka mashirika mbalimbali ya Jimbo Kuu la Arusha kwa ajili ya
kukata utepe wa uzinduzi.
http://www.mwananchi.co.tz
http://www.mwananchi.co.tz
ARUSHA.
MTU mmoja amefariki dunia na wengine 59 kujeruhiwa akiwamo Balozi wa Vatican na Mwakilishi wa Papa nchini Tanzania, Askofu Mkuu Francisco Montecillo Padilla jana asubuhi baada ya mtu asiyejulikana kurusha bomu wakati wa sherehe ya uzinduzi wa Jengo la Kanisa la Parokia ya Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, Olasiti, Arusha.

Miongoni mwa majeruhi, imeelezwa kuwa wanne ni mahututi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus
Sabas amelielezea kuwa tukio hilo kuwa ni la kigaidi hasa kutokana na
kumlenga Balozi wa Papa nchini na kwamba mtu mmoja anashikiliwa
akihusishwa nalo.
Wataalamu wa mabomu wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ) wanachunguza aina ya bo
mu lililotupwa lakini uchunguzi wa awali unaonyesha lilikuwa limetengenezwa kienyeji.
mu lililotupwa lakini uchunguzi wa awali unaonyesha lilikuwa limetengenezwa kienyeji.
Ilivyokuwa
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasimulia kuwa
bomu hilo lilirushwa yapata saa nne asubuhi wakati mgeni rasmi
akijiandaa kufungua jengo la kanisa baada ya ujenzi wake kukamilika.
Shambulio hilo lilitokea wakati balozi huyo akiwa
amesimama na mwenyeji wake, Askofu Mkuu, Josephat Lebulu, mapadri na
watawa kutoka mashirika mbalimbali ya Jimbo Kuu la Arusha kwa ajili ya
kukata utepe wa uzinduzi.
Kamanda Sabas alisema mtu aliyerusha bomu hilo
alitokea nyuma ya kanisa hilo la ghorofa na kurusha bomu hilo kwa mkono
wa kulia... “Alifanya jitihada za kupenya ili awafikie viongozi lakini
alishindwa kutokana na wingi wa waumini waliokuwapo kwenye eneo hilo.”
Padri Moses Mwaniki aliyemshikia Balozi Padilla
maji ya baraka yaliyotumika kubariki kanisa hilo, alisema kilichosaidia
bomu hilo kutomfikia mwakilishi huyo wa Papa ni kutua mgongoni mwa mmoja
wa waumini na kuanguka chini kabla ya kulipuka na kujeruhi watu.
“Ingawa hatuwezi kusema kwa uhakika, tunaamini
mlengwa mkuu alikuwa mgeni wetu, Balozi Askofu Mkuu Padilla. Tunatakiwa
kuliombea sana Taifa liondokane na matukio mabaya kama haya,” alisema
Padri Mwaniki.
Baada ya tukio hilo, Balozi Padilla, Askofu Lebulu
na viongozi wa kanisa hilo waliondolewa na kuhifadhiwa katika moja ya
vyumba vya kanisa hilo kabla ya kutolewa kwenye eneo hilo yapata saa
5.30 asubuhi chini ya ulinzi mkali wa polisi.
Msemaji wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Arusha,
Padri Festus Mangwangi alisema aliyerusha bomu hilo alishuhudiwa na
mtoto mdogo aliyekuwapo kanisani hapo.
0 comments:
Post a Comment