WAKATI ambapo Bongo5 inajiandaa kutoa orodha ya nyimbo 50 bora
zaidi kwa mwaka 2013, gazeti la Spoti Starehe limetoa orodha yake ya nyimbo 10.
“Video ya wimbo huu imepata watazamaji zaidi ya 1.5 milioni
tangu ulipowekwa You Tube kwa mara ya kwanza mwezi Septemba. Ni wimbo ulioweza
kumtambulisha Diamond kimataifa,” limeandika gazeti hilo.
“Alirekodi katika studio ya kawaida sana, Burn Records, lakini
wimbo huo umeweza kumkutanisha na mastaa wakubwa barani Afrika. Kwa mara ya
kwanza ameweza kufanya kolabo na Davido, Iyanya na wanamuziki wengine mashuhuri
barani Afrika.
Ameweza kutambulika kimataifa kutokana na video hiyo kuonyeshwa
katika televisheni nyingi Afrika sambamba na mahojiano.”
Nafasi ya pili imekatwa na single iliyomtoa Young Killa, ‘Dear
Game’.
“(Young Killer) amepata shoo nyingi, ni kijana mdogo aliyeibukia
katika Super Nyota 2012. Ameweza kuliteka soko na kupata shoo nyingi
zilizomwingizia kipato kikubwa,” limeandika.
Kwenye nafasi ya tatu, yupo Ommy Dimpoz na Tupogo, nafasi ya nne
ikienda kwa AY na FA na wimbo wao Bila Kukunja Goti waliomshirikisha J-Martins
huku nafasi ya tano ikienda kwa Nay wa Mitego na Diamond na wimbo wa Muziki
Gani.
Nafasi ya sita imekamatwa na Yahaya ya Lady Jaydee, ikifuatiwa
na Majanga ya Snura kwenye nafasi ya sababu, Roho Yangu ya Rich Mavoko
imekamata nafasi ya nane, Salam Zao ya Nay wa Mitego nafasi ya 9 na Utamu ya
Dully Sykes, Ommy Dimpoz na Diamond ikikamata nafasi ya 10.
0 comments:
Post a Comment