BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HII NDIYO SABABU YA BASI LA BURUDANI LENYE NAMBA YA USAJILI T 610 ATR KUPATA AJALI KISHA KUPINDUKA NA KUSABABISHA ABIRIA 12 KUFARIKI DUNIA KOROGWE-TANGA.



Ajali hii imetokea Leo korogwe mkoa Tanga inasadikika watu 17 wamepoteza maisha hapohapo.



WATU 12 wamekufa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria la Kampuni ya Burudani kutoka wilaya ya Korogwe mkoani Tanga kuelekea Jijini Dar es Salaam kuacha njia na kupinduka .


Ajali hiyo imetokea jana Disemba 12 majira ya saa 1.30 asubuhi katika Barabara Kuu ya Segera Chalinze eneo la Kwaluguru Kata ya Kwedizinga wilayani Handeni.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga Constantine Massawe alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha gari lenye namba za usajili T 610 ATR aina ya Nissan.


Kamanda Massawe alisema kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamefikishwa katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga kwa ajili ya kupata matibabu .


Alisema dereva wa ajali hiyo Luta Mpenda(35) ni miongoni mwa watu wanaosadikiwa kufa na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Korogwe ya Magunga.


“Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya magunga na hali zao bado siyo nzuri sana lakini na miili ya marehemu pia imehifadhiwa magunga”,alisema Kamanda Massawe.


Hata hivyo alisema kuwa chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa dereva wa basi hilo ambapo alipofika kwenye kona ya eneo la Kwalaguru gari lilimshinda na kupinduka.


Mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo akizungumza kwa shida katika Hospitali ya Magunga alikolazwa Francis Bendera alisema kuwa kulikuwa na gari aina ya Fusso iliyokuwa wagongane nayo uso kwa uso ndipo dereva wa basi alipojaribu kukwepa gari hilo na badala yake kona ikamshinda na kupinduka.


“Tukiwa tunakaribia kwenye kona ile kuna fusso iliover take kwa speed kubwa sana na ilikuwa ije kutugonga uso kwa uso sasa dereva wa basi letu akawa anajitahidi kukwepa sasa kutokana na ile kona kuwa kali ndipo gari ilimshinda na kupinduka”alisema Bendera.


Nao baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walisema kuwa walisikia kishindo kikubwa katika eneo hilo na ndipo walipokaribia kufika kwenye eneo la tukio walikuta tayari gari imeshapinduka na baadhi ya watu kufa papo hapo.


“Sisi tulikuwa tumekaa huku ghafla tulisikia kishindo kikubwa kuja kukimbia kuangalia ndiyo tukakuta Basi la Burudani limepinduka lakini ile gari ilikuwa igongane uso kwa uso na fusso kusema kweli ile ajali ni mbaya sana”,alisema Zablon Mbaga.


Hata hivyo baadhi ya wakazi wa wilaya ya Korogwe ambao walifurika katika hospitali ya Magunga kwa ajili ya kutambua miili ya ndugu zao na baadhi ya majeruhi waliofikishwa katika hospitali hiyo walisema kuwa idadi kubwa ya abiria waliokuwa wakisafari katika basi hilo ni wafanyabiashara.


“Wengi hapa ni wafanyabiashara ndio wanaotumia basi hili kwa sababu wanauhakika wakiondoka alfajiri saa 12 wanaweza kufika Dar mapema na kugeuza jioni”,alisema Fatuma Bakari mkazi wa wailaya ya Korogwe.


Mpaka sasa idadi ya majeruhi waliotokana na ajali hiyo imefikia 55 ambapo imemlazimu Mkuu wa Wilaya ya Korogwe,Mrisho Gambo kuanza zoezi la uhamasihaji wa utoaji damu kwa wananchi ili kuwanusuru wagonjwa hao ambao hali zao ni mbaya.


Akizungumza katika mahojiano na mtandao huu wa matukiodaima.com Gambo alisema kuwa majeruhi wengi wamepoteza damu nyingi hivyo mahitaji ya damu yamekuwa makubwa ukilinganisha na akiba iliyopo hospitalini hapo.


“Majeruhi wengi wamepoteza damu nyingi sana na sasa kilichopo tunahamasisha wananchi wajitolee damu ili tuweze kunusuru hali kwani ni mbaya sana”,alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya akiwa ni miongoni mwa watu wanaoshughulikia kuwapa huduma ya kwanza wagonjwa hao.


Hata hivyo alisema kuwa tayari majeruhi wanne wa ajali hiyo wameshasafirishwa kupelekwa katika Taasisi ya mifupi ya Moi kwa ajili ya matibabu zaidi.

Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: