Ndugu Zangu.
Nahitimisha simulizi za Mzee Wetu Madiba. Najisikia nimechukua jukumu
langu la kugawana nanyi kile kidogo nilichoweza kukusanya kumhusu Mzee
wetu Madiba.
Natumaini nitapata muda siku zijazo,
nisimulie zaidi juu ya yale yenye kufanya maisha ya Madiba kuwa simulizi
endelevu kwetu Waafrrika na watu wa dunia.
Lakini, ukweli unabaki, kuwa leo dunia imemzika Mzee Madiba kijijini
kwao Qunu. Yaliyobaki nyuma yake ni yale mema aliyoishi akayahubiri.
Nasi tunapaswa kujifunza kutoka hayo.
Yumkini Mungu amechagua
kupumzisha Mandela wakati muafaka. Maana, ni katika kipindi ambacho,
Afrika Kusini inaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwakani.
Chama kikuu cha ANC kinakabaliwa na changamoto za ndani ya chama na
kwenye jamii. Kinapaswa sasa kijiandae kufanya mabadiliko makubwa
yatakayorudisha imani ya wapiga kura wake wengi. Wapiga kura ambao
wameanza kukata tamaa. Hawana furaha ya maisha yao. Wamekata tamaa ya
kuona kuwa kesho yao yaweza kuwa bora zaidi.
ANC kihistoria imekuwa ikitegemea sana Jumuiya yake ya Vijana na
Shirikisho la Wafanyakazi ( Cosatu) Jumuiya zote hizo zinaonekana
kugawanyika. Kuna wanaoipa mgongo ANC.
Na Mandela anausia;
" The leader must keep the forces together, but you can't do that
unless you allow dissent. People should be able to criticise the leader
without fear of favour. Only in that case are you likely to keep your
colleagues together"- Nelson Mandela. It is when Mandela gave a piece of
advice to newly elected Party Leader, Thabo Mbeki at the ANC Congress
in Mafikeng, 1997.
Kwamba kiongozi unapaswa kuyaunganisha makundi, lakini, huwezi kufanya
hivyo kama huruhusu sauti kinzani. Sauti za wenye kukupinga. Watu wawe
huru kumshutumu kiongozi bila ya woga. Ni kwa namna hiyo tu kiongozi
unaweza kuyaunganisha makundi. Mandela aliyasema hayo kule kwenye
Mkutano Mkuu wa ANC uliompitisha Thabo Mbeki kuwa Rais wa ANC, ni mwaka
1977.
Naye Askofu Desmond Tutu alipata kusema;
"Kuna tofauti ya kimsingi kati ya kuwa huru na kuwa katika hali ya
kukandamizwa. Kuwa huru ni pamoja na kupata huduma za msingi za kijamii,
kuwa na ajira, maji ya bomba, umeme, makazi bora na huduma za msingi za
afya. Kuna maana gani basi ya kuwa huru wakati ubora wa maisha ya watu
haujaimarishwa? Kama sivyo, hata kura nazo hazina maana yoyote!"
(Desmond Tutu- William Gumede; Thabo Mbeki And The Battle For The Soul
Of The ANC, Uk. 67).
Nkosi Sikelel i Afrika!
Maggid Mjengwa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment