BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

HIVI NDIVYO SAFARI YA MWISHO YA NELSON MANDELA NA NAMNA ALIVYOZIKWA KIMILA KATIKA KIJIJI CHA QUNU.


Mazishi ya mzee Nelson Mandela yanaendelea muda huu katika kijiji cha Qunu katika mkoa wa Eastern Cape na kumaliza wiki moja ya maombolezi ya shujaa huyu wa Afrika mzee Nelson Mandela.



Idadi ya Takribani watu 4,500 wakiwemo wageni wa kimataifa wamehudhuria mazishi hayo yanayoendelea sasa hivi ambayo ni ya mchanganyiko wa tamaduni za kale na mambo ya kisasa. 



Familia ya Mandela ilikesha wakijiandaa kwa mazishi ya leo huku kukiwa na muimbaji ambaye atakuwa anaita mizimu ya mababu wa kale huku wakiongelesha mwili wa Mandela kumwambia kuwa sasa anazikwa.

RAIS WA TANZANIA AKIHOTUBIA.


Moja kati ya mataifa yaliyopata heshima ya kuongea mbele ya viongozi mbalimbali duniani ni Rais wa Tanzania mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete.


Eneo analozikwa mzee Nelson Mandela ni sehemu ya makaburi yaliyo kwenye shamba kubwa la familia ya Mandela lililoko katika kijiji cha Qunu lililojengwa mara baada ya kuachiliwa kutoka jela mwaka 1990, katika eneo lenye nyasi za kijani , na milima ya Cape ya mashariki.

Winnie Mandela



Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: