Hata hivyo, watafiti nchini Marekani wamebaini
kuwa wanawake wanaokunywa juisi ya nyanya angalau mara moja kwa wiki,
wanapunguza kiwango cha kupata maradhi ya saratani ya matiti.
Kwa mfano, wanaeleza kuwa glasi moja ya nyanya kwa
siku ina kiwango sahihi na cha kutosha cha madini ya Lycopene, ambazo
ni kemikali za mimea zinazoaminika kuondoa kukua kwa saratani.
Madini ya Lycopene ndiyo yanayozipa nyanya rangi
yake nyekundu na nyanya hizo zimeundwa zaidi ya vichocheo vyenye uwezo
wa kuzuia saratani hiyo.
Watafiti katika Chuo Kikuu cha Rutgers nchini
Marekani walipima, kiwango cha vichocheo kwa wanawake 70 wenye miaka 55
na kuendelea ambao walitumia juisi ya nyanya kwa wiki kumi. Wanawake
hao ambao wengi walikuwa wanene kupita kiasi na baadhi wenye dalili ya
saratani, walipungua uzito na saratani ilikwisha.
Kwa kuwa nyanya ni tunda linalopatikana wakati
wowote, tena jikoni kwako, ni vyema wanawake wakajenga mazoea ya
kuzitumia kama mlo hata wasipotengeneza juisi.
Imeandaliwa na Florence Majani, MWANANCHI.
0 comments:
Post a Comment