BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MAITI ILIYOKUTWA NA KETE 17 ZA MADAWA YA KULEVYA MOROGORO YAKABIDHIWA KWA FAMILIA.

Hivyo ndivyo maiti ilivyoPICHA ZOTE NA MTANDA BLOG
safirishwa kutoka Tundama mpaka Morogoro baada ya kukamatwa.
Askari kanzu akiichunguza maito muda mfupi kabla ya kutemshwa.

 maiti ya marehemu Khalid Kitala ikishushwa kutoka kwenye gari tayari kwa uchunguzi katika chumba cha kuhifadhia maiti.
Wahudumu wa chumba cha kuhifadhia maiti wakiandaa maiti muda mfupi kabla ya kuipasua tumbo na kutoa kete 17 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
Simu tano za wathumiwa zikiwa katika kituo kikuu cha polisi na kete 24 zinazodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya, kete 17 zilitolewa katika tumbo la marehemu baada ya kulipasua na kete sana zilikutwa katika gari ya watuhumiwa husika, Hizo kete zinazofanana na rangi ya njano ndizo zilizotolewa tumboni mwa marehemu
Kete saba ndizo zilizokutwa katika gari baada ya kupekuliwa.
Hii ndiyo gari iliyobeba maiti kutoka Tunduma kabla ya kukamatwa Mikumi Morogoro wakati ikielekea jijini Dar es Salaam na maiti.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoa wa Morogoro akihesabu kete, muda mfupi kabla ya Kamanda Faustine Shilogile kuongea na waandishi wa habari juu ya tukio hilo.
 
Huyu ndiye Kamanda Faustine Shilogile akiwaonyesha moja ya kete iliyotolewa tumboni mwa marehemu Khalid Kitala baada ya kusua tumbo kwa waandishi wa habari juu ya tukio hilo.

MAITI ILIYOKUTWA NA KETE 17 ZA MADAWA YA KULEVYA YAKABIDHIWA KWA FAMILIA
LILIAN LUCAS, Morogoro. 
MWILI wa aliyekuwa mfanyabiashara wa Kariakoo, Dar es Salaam, Khalid Kitara (47) uliokutwa na dawa za kulevya zinazodhaniwa kuwa ni heroini, umekabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya utaratibu wa mazishi.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa jana kwamba baada ya kufanyika kwa uchunguzi huo wameamua kukabidhi mwili huo huku wakiendelea na upelelezi kubaini mtandao unaohusika na tukio hilo.

Alisema jeshi hilo bado linaendelea kuwashikilia watuhumiwa watatu, ambao ni madereva wawili waliokuwa wakipokezana kuendesha gari hilo ambao aliwataja kuwa ni Teddy Sichilima (27), mkazi wa Tunduma Mbeya, Lucas Atubonekisye (32), mkazi wa Mtaa wa Songea, Tunduma na aliyekutwa na mwili wa Marehemu, Jumbe Mbano (36), mfanyabiashara na mkazi wa Kariakoo. Alisema watu hao watafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya uchunguzi kukamilika.

Alitoa wito kwa jamii kuendelea kuwafichua wahalifu ili sheria ichukue mkondo wake huku akisisitiza azma ya polisi kupambana kuhakikisha linatokomeza biashara ya dawa ya kulevya ambazo kwa sasa uuzaji wa dawa hizo umeonekana kuzagaa nchini.

MBARAONI WAKIDAIWA KUSAFIRISHA MADAWA YA KULEVYA WAKITUMIA MAITI.


Watuhumiwa Teddy Esco Sichirima (27) mkazi wa mtaa wa Mwaka-Tunduma, Lucas Atubonekisye Swila (32) mkazi wa mtaa wa Sogea Mbeya na Jumbe Hamad Mbano mfanyabiashara mkazi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam ndugu wa marehemu Khalid Abdul Kitala (47) wakiwa chini ya ulinzi eneo la chumba cha kuhifadhi maiti hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro.

 

NA LILIAN LUCAS, Morogoro. 
POLISI mkoani  Morogoro, wanawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kusafirisha maiti inayosadikiwa kuwa na dawa za kulevya.

Taarifa za vyanzo vya  kuaminika, zilisema  watuhumiwa walikuwa wakitokea Tunduma mkoani Mbeya  kwenda jijini Dar es Salaam.
Habari zilisema walipofika Mikumi, wilayani Kilosa  gari hilo lilisimamishwa na trafiki lakini dereva alikataa kusimamama.

Imeelezwa kuwa kitendo hicho kiliwapa mashaka trafiki  na kulazimika kulifuatilia  gari hilo lililokuwa katika mwendo mkali.
Kwa mujibu wa habari hizo baadaye askari waliamua  kufyatua risasi hewani, kitendo kilichowafanya watu hao kusimama.

Baada ya kusimama, askari walianza kuwahoji watu hao kuhusu hatua yao ya kukataa kusimama.

Inasemekana katika majibu yake mmoja wa watuhumiwa, alidai kuwa wanasafirisha maiti ya baba mkwe wake.

Ilidaiwa kuwa watu hao walikuwa wakisafiri na mtu huyo kabla hajafa   kwenda Zambia, lakini walipofika  Tunduma, alifariki dunia na baadaye watu hao waliamua kuirejesha maiti  yake  jijini Dar es Salaam kwa maziko.

Askari wa upelelezi wa  Kituo Kikuu cha Polisi cha mjini Morogoro, walionekana wakitoa  kete za dawa ya kulevya kutoka kwenye buti la gari. 


Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro, Dk Litha Lyamuya alisema mwili wa mwanaume    umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kukukutwa na vitu  vinavyofanana na pipi.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: