MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA YATOA TAHADHALI YA UWEPO WA MVUA KUBWA NCHINI.
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UCHUKUZI MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA
Simu: 255 22 2460735/2460706
FAKSI: 255 22 2460735/2460700 S.L.P. 3056
Barua pepe: met@meteo.go.tz DAR ES SALAAM
Tovuti: www.meteo.go.tz
Unapojibu tafadhali nakili:
Kumb. Na.: TMA/1622 12 Desemba, 2013
Taarifa kwa umma: Vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika maeneo ya nyanda za juu kaskazini-mashariki, ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na magharibi mwa nchi.
Taarifa Na. 201312-02
Muda wa Kutolewa
Saa za Afrika Mashariki
Saa 10 Jioni
Daraja la Taarifa: Tahadhari
Kuanzia: Tarehe 12 Desemba, 2013
Mpaka: Tarehe 13 Desemba, 2013
Aina ya Tukio Linalotarajiwa Vipindi vya mvua kubwa (zaidi ya mm 50 katika masaa 24 yajayo) katika maeneo yaliyotajwa hapo chini.
Kiwango cha uhakika: Juu (80%) Maeneo yatakayoathirika Baadhi ya maeneo ya nyanda za juu kaskazini-mashariki (Arusha, Manyara na Kilimanjaro), ukanda wa Ziwa Victoria (Kagera, Mwanza na Mara) pamoja na magharibi mwa nchi (Kigoma na Tabora).
MELEZO:
Hali hii inatokana na kuimarika kwa mfumo wa mgandamizo mdogo wa hewa ikiwa ni muendelezo wa ukanda wa mvua wa ITCZ.
Angalizo: Wakazi wa maeneo hatarishi wanashauriwa kuchukua tahadhari.
Maelezo ya Ziada Mamlaka ya Hali ya Hewa inaendelea kufuatilia hali hii na itatoa mrejeo.
Imetolewa na
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.
0 comments:
Post a Comment