Mwili
wa hayati Nelson Mandela umepelekwa katika mkoa wa Eastern Cape kwa
safari ya mwisho kabla ya kuzikwa siku ya Jumapili kijijini Qunu.
Idadi kubwa ya watu walifurika barabara angalau kumtupia jicho shujaa wao na kutoa heshima zao za mwisho.
Mandela aliyefariki tarehe tano Disemba atafanyiwa maziko ya kitaifa siku ya Jumapili,
Takriban
watu 100,000 walitoa heshima zao za mwisho kwa Mandela mjini Pretoria
siku ya Ijumaa kabla ya mamia ya wengine kukosa fursa hiyo pale
walipokatazwa kumuona Mandela kutokana na ufupi wa mda.
Kijiji cha Qunu.
Kijiji
cha Qunu ambako atazikwa Hayati Nelson Mandela, kinaomboleza kifo cha
shujaa aliyetoka katika kijiji hicho Nelson Mandela.
Mazingira hapa ni ya kipekee, mchanganyiko wa nyumba za kisasa na za kitamduni ambazo mfano wake ni mizinga ya Nyuki.
Visima
vya maji anavyovikumbuka Mandela bila shaka hawezi kuviona sasa. Lakini
viwanja vya kijiji hiki viko chini ya majabali ambayo yeye na rafiki
zake walikesha wakichezea.
Ni viwanja hivi ambapo Madiba
alijifunza kuwinda Ndege , kuchukua asali misituni na matunda ya misitu
ambayo ilikuwa inaliwa wakati huo.
Alipokuwa na umri wa miaka 5,
Mandela aliandika kumbukumbu zake kuhusu safari yake alivyopigania uhuru
wa Afrika Kusini, pia alijifunza kuchunga Ng’ombe, na kupitia kwa kazi
hiyo alijifunza uhusiano uliopo kati ya watu wa kabila la AbaTembu na
Ng’ombe wao.
Alisomea hapa Qunu, lakini kijiji alichokiacha kwa
huzuni wakati alimzika babake kimebadilika. Lakini aliporejea hapa mwaka
1990 alipokuja kutembelea kaburi la mamake , alisema aliona umasikini
mkubwa machoni mwa watu wa Qubu, viwanja visafi alivyovikumbuka
havikuwepo tena, vilikuwa vimejaa takataka kitu ambacho hakuwahi kukiona
tangu alipokuwa mtoto.
Hata hivyo Kijiji cha Qunu bila shaka
kimebadilika pakubwa, ni kisafi kikubwa na kina dalili za maendeleo,
wala sio taswira aliyoitoa Mandela katika kumbukumbu zake kuhusu
nyumbani.
Na sababu moja ya hilo ni kuwa alijenga nyumba hapa
pamoja na shule, alilemaji, umeme, pamoja na mapato kwa watu wa eneo
hili kutokana na makavazi aliyojengewa Mandela ambako atazikwa.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment