SERIKALI imewasafisha aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo huku ikimpandisha cheo aliyekuwa Mganga Mkuu wa Serikali Deo Mtasiwa.
Nyoni alisimamishwa kazi pamoja na aliyekuwa
Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa na wote kwa pamoja walikuwa na
tuhuma za kutumia vibaya madaraka yao wakiwa watumishi wa umma.
Jairo kwa upande wake alisimamishwa kazi kutokana
na kuchangisha fedha kinyume cha sheria kwa lengo la kusaidia mchakato
wa kupitisha bajeti ya wizara yake, katika mwaka wa fedha 2011/2012 na
sasa ameondolewa kwenye utumishi wa umma, huku Bunge likiwa bado
halijapata taarifa ya utekelezaji wa maazimio yanayomuhusu.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa Nyoni kwa
sasa amerejea kwa mwajiri wake wa awali, Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA), akishikilia nafasi ya mmoja wa wakuu wa idara, huku Dk Mtasiwa
akiwa ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, katika Ofisi ya Waziri Mkuu,
Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa (Tamisemi).
Katibu Mkuu Kiongozi
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amelithibitishia gazeti hili kuhusu watumishi hao na kwamba taratibu zimefuatwa.
“Mimi ninachojua ni kwamba Blandina alikuwa
mwajiriwa wa TRA na mkataba wake ulikuwa haujaisha… Siyo kwamba alikuwa
na mikataba miwili, kwenye utumishi wa umma huwa kuna utaratibu wa
kuazima watumishi wa umma.
Ndiyo maana unaweza kukuta mwanajeshi anatolewa
jeshini na kupelekwa uraiani au mtumishi kutoka idara moja kwenda
nyingine. Kwa upande wetu sisi tulishamwondoa kwenye ukatibu mkuu na
kule TRA hakuwa na tatizo,” alisema Balozi Sefue.
Kuhusu Dk Mtasiwa alisema: Uteuzi wa Dk Mtasiwa
ulikuwa wazi na hata alipoapishwa mambo yote yalitangazwa hadharani.”
Aliendelea kufafanua kuhusu Jairo akisema: “Jairo alishaondolewa kwenye ukatibu mkuu, siyo mtumishi tena wa umma.” Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alimtetea Nyoni akisema kuwa amerudi kwenye ajira yake ya awali.
Aliendelea kufafanua kuhusu Jairo akisema: “Jairo alishaondolewa kwenye ukatibu mkuu, siyo mtumishi tena wa umma.” Naye Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo alimtetea Nyoni akisema kuwa amerudi kwenye ajira yake ya awali.
“Siyo kwamba ameajiriwa TRA, amerudi tu kwenye
ajira yake ya zamani, alikuwa akifanya kazi hapa akaazimwa na sasa
amerudi,” alisema Kayombo na kuongeza: “Kwani amefanya kosa gani? Kuna
mashtaka yoyote aliyofanya unaweza kuyathibitisha?”
Kauli hiyo iliungwa mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya
TRA, Bernard Mchomvu ambaye alisema Nyoni alishasafishwa na Serikali
ndiyo maana wamempokea. “Yule aliazimwa tu na Serikali…Sasa kama
Serikali imesham-clear sisi tutamkataaje?” alihoji na kuongeza:
“Kwa sababu sikumwomba huyo mtu, nimeambiwa kwamba
huyo yuko safi mimi nifanyeje? Unajua watu wanafurahia wengine wakipata
matatizo, hata kama mtu ameua, basi walete ushahidi.
Hata unaposema nchi imejaa rushwa, ulete ushahidi… kama Serikali imeshamsafisha, ningemkataa ningekuwa mtu wa ajabu.”MWANANCHI
Hata unaposema nchi imejaa rushwa, ulete ushahidi… kama Serikali imeshamsafisha, ningemkataa ningekuwa mtu wa ajabu.”MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment