Uchomvu isiwe sababu ya kunyimana ‘chakula cha usiku’.
Ndani ya maisha ya ndoa, muda wowote mwenzako anapohitaji penzi hutakiwi kumkatalia kwa kuwa wewe ndiye daktari wake na kumkubalia kwako ni sawa na kumtibu ugonjwa ambao ungeweza kuyaathiri maisha yake.
Hata hivyo, asilimia kubwa ya wanandoa wanatajwa kufanya tendo la ndoa wakati wa usiku. Usiku wa saa ngapi? Hiyo itategemea na wanandoa husika.
Lakini sasa inaelezwa kuwa wanandoa wanaofanya
kazi ni vigumu sana kulifurahia tendo la ndoa kwa kulifanya usiku. Hii
ni kwa sababu, muda huo kila mmoja anakuwa amechoka kutokana na
mihangaiko ya siku nzima.
Usiku ni tatizo?
Wanaume
wengi wakati wa usiku ndiyo wanautumia kutafakari juu ya maisha, pia
ni wakati ambao wanakuwa wamechoka hivyo wanaweza kukosa mshawasha wa
kukutana na wake zao.
Ukijaribu kufuatilia utabaini ndoa nyingi
ziko kwenye migogoro chanzo kikiwa na wanawake kutopatiwa haki zao za
ndoa. Wanaikosa haki hiyo kwa kuwa muda ambao waume zao wanatakiwa
kuwapa ‘mambo’, wanakuwa hoi.
Mbaya zaidi baadhi ya wanawake
hufikia hatua ya kuhisi wanasalitiwa kumbe siyo kweli bali inatokana na
kutopatiwa raha hiyo kwa wakati walioutarajia.
Wataalam wa
mapenzi wanaeleza kuwa, usiku ndiyo muda muafaka kwa wanandoa kukutana
na kwa mwanaume hata kama atakuwa anajisikia hali ya kuchoka, ajue ana
wajibu wa kufanya hivyo.
Kufanya mapenzi ni moja ya mazoezi hivyo
mwanaume anaporudi nyumbani asikimbilie kuoga, kula na kulala bali
akumbuke kumpatia haki mke wake, haki ambayo pia inamsaidia kimazoezi.
Inaelezwa
kuwa, mwanaume kujihisi uchovu kila siku na kushindwa kufanya tendo la
ndoa ni dalili kwamba ana tatizo la kiafya analotakiwa kulitafutia
ufumbuzi haraka kabla ya kuiathiri ndoa yake.
Mapenzi ni starehe
Ifahamike
kwamba, kufanya mapenzi licha ya kwamba unatumia nguvu na akili lakini
ni sehemu ya kustarehe. Ndiyo maana wengine baada ya kumaliza shughuli
zao za siku nzima badala ya kwenda baa, moja kwa moja wanakwenda
nyumbani na wakifika huko wakioga wanaweza kutumia muda mwingi kitandani
na wenza wao.
Kwa maana hiyo kukutana faragha isichukuliwe kama
kitu kitakachokufanya uzidi kuchoka bali kwa kutumia kanuni sahihi,
uchovu hauwezi kuwa sababu ya kutomtimizia mwenzake haki yake ya ndoa.
Mwanaume afanyeje?
Zipo
njia mbalimbali za kukabiliana na hali ya uchovu na leo nitazungumzia
mbili ambazo naamini ukizifanyia kazi zinaweza kukusaidia.
Kunywa kahawa
Wapo
wanaoitumia kama njia ya kuwafanya wasilale usiku lakini pia kitaalam
inaelezwa mtu anapokunywa kahawa kabla ya kupanda kitandani inamsaidia
kuondoa uchovu.
Aidha, kahawa ina uwezo wa kumfanya mtu apate
mshawasha wa kufanya tendo la ndoa hata kama ametoka kwenye kazi
zilizomfanya achoke sana.
Mazingira ya kutokuwa mchovu yatamfanya
aweze kumtimizia mke wake haki yake ya ndoa bila wasiwasi. Cha
kuzingatia katika hili ni kunywa kahawa kiasi ili isikuletee madhara
badala ya faida.
Tumia zabibu za baridi
Wataalam
wanaeleza kuwa, zabibu hasa za baridi zinaweza kukuweka katika
mazingira mazuri ya kukutana faragha na mwenzako na kushibishana
chakula cha usiku.
Ukiwasili nyumbani kutoka kazini na kuhisi
hali ya kuchoka. Baada ya kuoga ukiwa umepumzika kula tunda hilo
taratibu, faida yake utaiona utakapokuwa kitandani na mwenza wako.
Zingatio
Kukutana
faragha ni mhimili muhimu katika kuidumisha ndoa. Visingizio visivyo
na msingi visitumike kunyimana utamu huu. Kama umechoka basi ujue
ukifanya mapenzi na mwenzako uchovu utaondoka, kama hujisikii kufanya
hivyo mwenzako atakupa stimu lakini usipuuzie hisia zake.
MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO
Home / Uncategories / UCHOVU ISIWE SABABU YA KUMNYIMA MWENZIO PENZI, TABIA HII WANAUME NDIYO WAMEKUWA WAKIENDEKEZA NA KUMNYIMA FULSA MWANAMKE YA KUKIDHI HAJA YAKE.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment