BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

UTII WA SHERIA BILA SHURUTI NAMNA UNAVYOTATIZA RAIA WA TANZANIA PENGINE NA DUNIA.

TUKIO HILI LILIJITOKEZA DES 7/ 2013.
Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Pascal Mwakambungu kushoto akitafuta mbinu za kumsua dereva wa daladala zinazofanya kazi ya usafirisha abiria kati ya Kihonda na mjini katika bomba za daraja la mto Morogoro kufuatia dereva huyo kugoma kwenda kituo cha polisi baada ya kudaiwa kuvunja sheria za usalama barabara katika stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro kwa kuegesha daladala eneo isiyoruhusiwa na kusabaisha foleni iliyoziba barabara kuu endayo ofisi za mkuu wa mkoa wa Morogoro mkoani Morogoro.PHOTO/ MTANDA BLOG.
NI kama anamweleza hivi hapa lazima uende tu kituo cha polisi hivyo tii sheria bila shuti, lakini inaonekana mambo hayakuenda vyema na kulazimika nguvu itumike kidogo kumtoa eneo hilo.PHOTO/ MTANDA BLOG.AKATEKELEZA: utii wa sheria nila shuruti safari ikaanza kuelekea kituo.PHOTO/ MTANDA BLOG.
MWANDISHI wa gazeti la JAMBOLEO mkoa wa Morogoro, Peter Kimath (fulana ya njano) ambaye ni Shabiki mkubwa wa klabu ya Manchester United akifuatilia tukio hilo kwa ajili ya kupata habari.
PHOTO/ MTANDA BLOG.
BAADA YA ASKARI KUOMBA MSAADA WA GARI NA KUSIMAMA: Dereva huyo alifanya mgomo wa kutii sheria bila shuruti kwa kukataa kuelekea kwenye gari hilo na tena msobemsobe ulianza tena na kupandishwa kwenye gari hilo.
PHOTO/ MTANDA BLOG.

Mkaguzi Msaidizi wa Polisi, Pascal Mwakambungu kushoto akisimamia zoezi la kupindwa kwa dereva wa daladala zinazofanya kazi ya usafirisha abiria kati ya Kihonda na mjini kupanda katika gari la polisi baada ya dereva huyo kudaiwa kuvunja sheria za usalama barabara katika stendi kuu ya daladala yaendayo nje ya Manispaa ya Morogoro kwa kuegesha daladala eneo isiyoruhusiwa na kusabaisha foleni iliyoziba barabara kuu endayo ofisi za mkuu wa mkoa wa Morogoro mkoani Morogoro.PHOTO/ MTANDA BLOG.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: