BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

WAKAZI WA DAR ES SALAAM WATUMIA VITUO VYA MABASI YAENDAYO KASI KUGEUZA KUWA NYUMBA ZA MAGANGURU KUFANYA NGONO, WATEJA HUTOZWA KIASI CHA SH3,000 HADI SH5,000 TU.

DART 
BAADHI ya wakazi wa Dar es Salaam wanatumia vituo vya mabasi yaendayo kasi (DART) kama madanguro ya kufanyia ngono na sehemu za uporaji  kwa vijana wa kihuni. 



Uchunguzi wa Tanzania Daima umebaini vitendo vya ngono zembe vinafanywa na wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili yao kwenye vituo hivyo hasa sehemu za Magomeni, Manzese na Ubungo.


Eneo la Magomeni Mapipa ndilo lililoshamiri kwa vitendo vya ngono kuanzia majira ya usiku hadi alfajiri.
Mbali na vitendo vya ngono, pia kumekuwa na matukio ya uporaji na ukabaji hasa kwa wakazi wanaopita maeneo hayo.


Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa vijana wanaouza bidhaa ndogo ndogo jirani na kituo cha Magomeni Mapipa, Joseph Mwalingo, alisema vitendo vya ngono vimeshamiri eneo hilo hasa baada ya kujengwa kwa kituo hicho.


“Hii biashara si ngeni hapa, awali hawa wanawake walikuwa wakisimama kusubiria wateja wao, na kufanyia vitendo vyao katika jengo moja la ghorofa maarufu Kwa Babu, lakini baada ya kituo kujengwa naona wengi wanafanyia hapa hapa,” alisema Joseph.
Joseph alisema amekuwa akipata faida  kutokana na kuwauzia wanawake hao vitu mbalimbali ikiwemo sigara na kondomu.


Tanzania Daima ilishuhudia vitendo hivyo kwenye kituo hicho ambapo wahusika utandika boksi huku pembeni wakiziba kwa khanga zinazopita kati ya nguzo zilizopo kwenye vituo hivyo kwa malipo ya kuanzia sh 3,000 hadi 5,000.


Inadaiwa endapo watafanyia tendo hilo Kwa Babu, mteja atatakiwa kutoa sh 1,000 kama malipo ya eneo na kama watafanyia hapo kituoni inakuwa ni maelewano ya wawili bila pesa ya ziada.
Aidha, gazeti ili lilishuhudia kuwapo kwa walinzi wanaolinda eneo la kituo, lakini hakuna juhudi zozote zinazochukuliwa.


Mmoja wa wanawake alipoulizwa juu ya usalama kwenye eneo hilo, alisema ulinzi wa kutosha upo na kwamba wanawatumia vijana wa kiuni wanaoshinda jirani na vituo hivyo.


Mbali na vituo hivyo, pia gazeti hili lilipata kutembelea maeneo kadhaa ya vituo hivyo ikiwemo Kagera, Manzese, Tip Top na Stendi ya Kituo cha Mabasi ya Mikoani Ubungo, ambako baadhi ya vituo ilishuhudia watu mbalimbali wakiwa wamelala. TANZANIA DAIMA.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: