Kijana kulia akimwonyesha simu mwendesha baiskeli kwa lengo la kutaka kumuuzia, kundi la vijana wanadhaniwa kuwa ni vibaka hutanda kando ya barabara ya Sabasaba kuanzia stendi ya Mzumbe hadi kanisa la Anglikana kwa kuwaibia wapita njia kwa kuwauzia vipande vya sabauni badala ya simu wakati mnunuzi akijiandaa kutoa pesa baada ya maelewano.PHOTO/MTANDA BLOG
Hatua hiyo hutumiwa vyema na vibaka hao kubadilisha simu halali na kumwewekea mteja wao kipande cha sabuni kilichohifadhiwa vizuri katika bahasha ya kaki jambo ambalo baadhi ya watu wenye uelewa mdogo wamekuwa wakiibiwa kwa mfumo huo, kazi hiyo hufanywa kila siku ya mungu na vijana hao na baada ya wiziki huo hutoweka na wanaporudi tena eneo hilo tayari wamebadilisha mavazi na kuwa kero kwa wakazi wasamalia wema.
BLOG ya jamii ya MTANDA BLOG imeshuhudia vitendo vya uhalifi vikifanywa na vijana hao na kufanikiwa kunasa baadhi ya picha za matukio yao yakifanywa mchana kweupe achilia mbali yale ya uskiku ambayo hayana utetezi.
Vijana hao wamekuwa wakali hasa pindi mteja wao anapobaini ameibiwa na wamekuwa na ushirikiano mzuri na inafikia hatua mteaja wao anahitaji kurudishiwa pesa basi yupo katika hatari ya kuweza kupigwa pengine kuondoka na majeraha mwilini mwake kutokana na umoja wao.
0 comments:
Post a Comment