BREAKING NEWS !!!!!! WATU 13 WAFARIKI DUNIA KATIKA AJALI YA NOAH SINGIDA.
Habari zilizotufikia sasa hivi kutoka Singida zinasema watu 13 wamefariki dunia baada ya kutokea ajali ya magari mawili kugongana uso kwa uso eneo la Isuna mkoani humo.
Habari zinasema ajali hiyo ilihusisha gari aina ya Toyota Noah na lori ambayo namba zake za usajili hazikupatikana mara moja. Watu 13 waliofariki walikuwa katika Noah iliyokuwa ikitokea Itigi na maiti zao zimehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Singida.
Baada ya ajali hiyo, dereva wa lori na msaidizi wake walitokomea kusikojulikana.
0 comments:
Post a Comment