IRINGA.
MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amesema kama Rais Jakaya Kikwete anadhamira ya kweli kutokomeza ujangili nchini ni vyema akasafisha kwanza Serikali na chama chake.
MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amesema kama Rais Jakaya Kikwete anadhamira ya kweli kutokomeza ujangili nchini ni vyema akasafisha kwanza Serikali na chama chake.
Akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika Viwanja
vya Mwembetogwa mjini hapa juzi, Mchungaji Msigwa alisema kasi ya
ujangili ni kubwa na baadhi ya wahusika ni vigogo ndani ya CCM.
Alisema wengine wanatoka serikalini hususan
jeshini; Idara ya Usalama wa Taifa na Polisi jambo linalosababisha
operesheni hiyo kuwa ngumu kwa utekelezaji.
Alisema hali hiyo ndiyo chanzo hata cha Operesheni Tokomeza Ujangili iliyositishwa kwa muda kupoteza mwelekeo.
“Tulipoanza kupiga kelele juu ya vitendo vya
ujangili tuliambiwa tunataka umaarufu kisiasa, lakini hali ilipofikia
wao wenyewe wamekubali na kuanzisha hata Operesheni Tukomeza Ujangili,
lakini niliwaambia mtandao wa ujangili ni mkubwa,” alisema Mchungaji
Msigwa na kuongeza:
“Unahusisha vigogo ndani ya CCM, si mnakumbuka
niliwahi kuwatajia majina na kuwaambia wawekwe mbali na Tembo... baadhi
yao ni polisi wengine ni wanajeshi, kama kweli Rais Kikwete ana nia ya
dhati kupambana na ujangili ni vyema akasafisha nyumba yake kwanza.”
Mchungaji Msigwa alisema Serikali ilianzisha
Operesheni Tokomeza Ujangili kwa nia njema, lakini kwa sababu majangili
wanatoka ndani ya Serikali hivyo imekuwa vigumu kufanikisha kazi hiyo.
Alisema ndiyo sababu hata malengo yake yalipotoshwa, huku walengwa wakiachwa na kuanza kuua raia wasio na hatia.
Alisema ndiyo sababu hata malengo yake yalipotoshwa, huku walengwa wakiachwa na kuanza kuua raia wasio na hatia.
Mbunge huyo alisema hivi sasa kasi ya ujangili
inatisha na kuongeza kuwa, kwa siku zaidi ya Tembo 60 wamekuwa wakiuawa
jambo linalowafanya wanyama hao muhimu kuwa hatarini kutoweka.
Alisema hatua ya mawaziri wanne kujiuzulu
inaonyesha dhahiri wabunge wa upinzani na Bunge kwa jumla limetekeleza
wajibu wake na kwamba, hiyo inatosha kujiaminisha kwa wapigakura wao.
Hata hivyo, Msigwa alisema msimamo wake ni kwamba
Serikali ina viongozi mzigo, huku akimtaja Waziri Mkuu, Mizengo Pinda
kuwa ni kiongozi mzigo. MWANANCHI
0 comments:
Post a Comment