BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

ILIYOVUMA MWAKA 2013 NDIYO HII NA KUVUTA HISIA, HUYU NDIYE SHEIKHE ALIYEKAMATWA KISHA WAISLAM WAKACHANGA SH6 MILIONI KAMA DHAMANA KUFUTIA KUTIWA NGUVUNI NA POLISI MKOANI TABORA.


Sheikhe Ilunga Hassan Kapungu.


Kutoka gazeti la Annuur-Ijumaa-Desemba 20-25/2013.
Na Bakar Mwakangwale
SHEIKHE Ilunga Hassan Kapungu wa Mwanza amekamatwa mjini Tabora siku ya Ijumaa tarehe 13 Desemba 2013 akiwa nyumbani kwa dada yake.


Sheikh Ilunga alirudi nchini Oktoba 15,2013 kutokea India alikokuwa akipatiwa matibabu. Alikaa jijini Dar es Salaam kupumzika kwa wiki mbili baadae akaenda nyumbani kwake Mwanza.Wiki iliyopita alikwenda Tabora kwa ajili ya kumjuilia hali bibi yake na ndugu wengine wa kifamilia.



Ijumaa aliyokamatwa alikuwa amekwenda kwa dada yake na ndipo polisi kutoka Mwanza walipofika na kumkamata.Alifikishwa kwenye kituo cha polisi mjini humo kwa mahojiano.Baada ya mahojiano hayo alitakiwa kupelekwa jijini Mwanza kwa ajili ya kufikishwa mahakamani.



Waislamu wa Tabora wakiongozwa na sheikh Abdulhafidh Saburi walifanya makubaliano na polisi ili asipelekwe Mwanza akiwa chini ya ulinzi wa polisi kulingana na afya yake.Katika makubaliano hayo alitakiwa afike kwa RPC wa Mwanza siku ya Jumatatu.Kulingana na ushahidi wa vyeti vya matibabu vya sheikh huyo, ilikubaliwa aanze kuonana na daktari wake kama ilivyopangwa siku hiyo ya Jumatatu ndipo aripoti polisi.



Ilipofika saa 5 asubuhi sheikh Ilunga alifika kwa RPC wa Mwanza .Baada ya mahojiano alitakiwa kufikishwa mahakamani lakini ikashindikana kwa vile jalada la kesi yake lilikuwa bado liko kwa mwanasheria wa serikali na ikabidi arudi siku ya Jumanne kufikishwa mahakamni.



Katika kesi hiyo sheikh Ilunga ameshtakiwa kwa makosa matatu yote yatokanayo na maudhui ya maneno kwenye CD na DVD za mihadhara yake aliyotoa sehemu mbali mbali nchini.



La kwanza ni kusema kuwa serikali ilikuwa ikichota mamilioni ya fedha kuyapa makanisa.Shtaka la pili ni kusema Nyerere aliyekuwa rais wa kwanza Tanzania alikuwa akihujumu waislamu na hata kuwauwa ili ukristo uchukue nafasi.Na shtaka la tatu ni kusema kuwa akiuliwa sheikh basi akamatwe na padre naye auwawe.

Akiongozwa na mawakili wake wawili sheikh Ilunga alikanusha mashtaka yote matatu.Awali wakili wa serikali alitaka sheikh Ilunga asipatiwe dhamana.



Hata hivyo kutokana na utetezi wa mawakili wake,dhamana ilitolewa chini ya masharti magumu moja wapo likiwa ni kupatikana kwa wadhamini wawili wa shilingi milioni tatu tatu taslimu.Kwa vile waislamu walikuwa wamejitayarisha masharti yote likiwamo hili yalitimizwa na mshtakiwa kuwachwa huru mpaka tarehe 16 Januari 2014 kesi itakapoendelea.

Baada ya kutoka mahakamani waislamu walikushanyika Gandiholi ambapo sheikh Ilunga aliwasalimia tu waislamu bila kuzungumza lolote la ziada.Kiongozi wa kamati ya kushughulikia kesi za waislalmlu jijini humo,Imamu Hamza alikanusha taarifa potofu za vyombo vya habari kuwa sheikh Ilunga alikamatwa akiwa mafichoni mjini Tabora.
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: