BannerFans.com

MBUNGE SUZAN KIWANGA AKWAMISHA KESI MAHAKAMANI MOROGORO

MANYANYASO YAKITHIRI SUDAN KUSINI.




Wa-Sudan Kusini waliokoseshwa makazi
Watu waliokoseshwa makazi kutokana na mapigano katika mji wa Bor baada ya kuwasili katika bandari ya Minkaman, nchini Sudan Kusin.
AFISA mwandamizi wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa amesema jumatatu kwamba maelfu ya watu wameuawa katika ghasia huko Sudan Kusini na baadhi ya ukiukaji mbaya sana wa haki za binadamu huenda ukapelekea kuwepo kwa uhalifu wa vita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.


Katibu mkuu msaidizi wa masuala ya haki za binadamu, Ivan Simonovi amelitembelea taifa hilo lililogubikwa na mzozo wiki iliyopita. Amesema hali ni ya kusikitisha sana na kuelezea orodha ndefu ya manyanyaso  ikiwemo mauaji, uchinjaji holela, ghasia za ngono, uchomaji, wizi wa ngawira na matumizi ya wanajeshi watoto.
Bwana Simonovic amesema ana matumaini kwamba katika muda wa wiki kadhaa watatoa ripoti ambayo itakuwa na baadhi ya matokeo ya awali kuhusu uchunguzi uliofanywa. Hadi sasa anasema kuna baadhi ya ushahidi  na wana baadhi ya tuhuma ambazo hazijafanyiwa uchunguzi wa kutosha.

Tayari anasema kwamba pande zote zimehusika na matukio ya ukiukaji wa haki za binadamu.Simonovic amesema ripoti yake ya awali huenda isiweze kuwatambua wanaotuhumiwa kutenda maovu  ambayo wakati mwingine itachukua muda zaidi.

Pia amesema kwamba Umoja wa Afrika-AU imependekeza kwa tume ya uchunguzi kuchunguza ukiukaji na kuzungumzia kiini cha mzozo.


Wa-Sudan Kusini waliokoseshwa makaziWa-Sudan Kusiniwaliokoseshwa makazi

Ghasia zilizuka katika taifa hilo changa katikati ya mwezi Disemba  wakati Rais Salva Kiir alipomshutumu naibu wake wa zamani Riek Machar kwa jaribio la mapinduzi, dai ambalo Machar amelikanusha.

Tangu wakati huo  mzozo umegeuka kuwa ghasia za kikabila ambazo zimehusisha makabila ya Nuer na Dinka na kusababisha vifo pamoja na raia kadhaa kukoseshwa makazi. http://www.voaswahili.com
Share on Google Plus

About mtanda blog

Blogger maarufu nchini Tanzania na mwanahabari mkongwe kwenye Tasnia ya habari
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: